Wanafunzi watatu wafariki kwa kufukiwa na kifusi cha mchanga


Wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Mbori wilayani Mpwapwa wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba mchanga kwenye korongo.

Inadaiwa kuwa wanafunzi hao walitumwa mchanga huo na walimu wao.

Akizungumzia tukio hilo jana, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Josephat Maganga, alisema tukio hilo limetokea saa tatu asubuhi na limeacha maswali mengi ya kujiuliza.

Aliwataja wanafunzi waliofariki ni Rehema Alex ambaye anasoma darasa la nne, Daudi Machea wa darasa la tano na Ezla Lucas wa darasa la sita.

Waliojeruhiwa Arafa Athumani(10), Nelly Daudi(12), wilsoni Amosi, Yunis Mussa(12), mwijuma machimo(13),

“Kuna maswali ya kujiuliza walienda peke yao? nani aliwatuma? Je, ilikuwa ni wakati wa vipindi vya darasani? Kuwatuma mchanga kwenye mto na kokoto tumepiga marufuku,”alisema.

Alibainisha kuwa kazi za maendeleo kwa maelekezo ya serikali zimeachwa kwa wazazi ndio watakaa na kupanga wenyewe.

Amesema uchunguzi unafanyika na wote waliosababisha tukio hilo watachukuliwa hatua.


from MPEKUZI

Comments