Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ....Mwigulu Nchemba Kawa Waziri wa Fedha


Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri Tanzania

Rais  Samia suluhu Hssan  ametaja mabadiliko hayo mapya ya baraza hilo  jipya la mawaziri wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

Mawaziri hao ni  kama ifuatavyo;, Rais Samia Suluhu Hassan amemhamisha aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), huku aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Seleman Jaffo akipelekwa kushika nafasi ya Ummy Mwalimu.

Mwigulu Nchemba amepelekwa wizara ya Fedha na Mipango akisaidiwa na Hamad Masauni na nafasi yake katika Wizara ya Katiba na Sheria kuchukuliwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akisaidiwa na Jofrey Mizengo Pinda.

Balozi Liberata Mulamula ameteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, huku naibu wake akiteuliwa Mbarouk Nassoro Mbarouk.

Kwa upande wa Wizara ya Nchi ofisi ya Rais, utumishi na Utawala bora, ameteuliwa Mohamed Omary Mchengelwa, huku aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Capt. George Mkuchika akipangiwa kazi nyingine.

Wizara ya Uwekezaji imerejeshwa katika ofisi ya Waziri Mkuu na kutolewa ofisi ya Rais, huku Godrey Mwambe akiteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo na Prof. Kitila Mkumbo akipelekwa wizara ya Viwanda na Biashara.

Pauline Gekul ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa wizara ya Michezo, Sanaa, Utamaduni na Michezo, huku aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo, Abdallah Ulega akipelekwa wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa naibu waziri.

Naye, Mwanaidi Ally Hamis ameteuliwa kuwa naibu waziri wa pili katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 

Akitangaza mabadiliko hayo, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kuondoka kwa Dk. Philip Mpango katika Wizara ya Fedha na Mipango kumempa nafasi ya kulitazama baraza lote la mawaziri na kufanya mabadiliko kidogo.

Katika upande mwingine, Rais Samia amefanya uteuzi wa wabunge watatu ambao ni Dk. Bashiru Ally, Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk

Zaidi , Tazama Video hapo chini



from MPEKUZI

Comments