Watu Wanne Watiwa mbaroni kwa Kueneza Uvumi Na Kutia Hofu Wananchi Kuhusu Corona


 Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutumia mitandao ya kijamii kueneza uvumi wa vifo vya watu wakidai wamefariki kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema uzushi huo umewatia hofu na taharuki wananchi.

Akizungumzia tukio hilo amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni hao ni Frank Nyange (47), Mozes Mgao (34) Mohamedi Lutambi (47) na Bumija Senkondo (55).

“Watuhumiwa hawa wanne tuliowakamata na wengine ambao tunaendelea kuwatafuta wanasambaza taarifa za uvumi za vifo vya Watu wakidai wamekufa kwa Corona na pia wanapendekeza majina ya Viongozi wa Serikali ambao walitamani wafe haraka kwa Corona

“Watuhumiwa hawa wanne tunaowashikilia Frank Nyange na wenzake, pamoja na wengine ambao tunawatafuta, licha ya kueneza uvumi wa vifo vya Watu wakidai wamekufa kwa Corona, pia wanatia hofu Mitandaoni kwa kudai Watanzania walio wengi watakufa kwasababu Serikali haichukui tahadhari dhidi ya Wananchi wake

“Polisi Mkoani Pwani tunatoa rai kwa Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya na kujiepusha na matumizi mabaya ya Mitandao ikiwemo kutoa taarifa za uvumi kuhusu vifo vya Watu ambazo zinatia hofu Wananchi wengi, hatua za Kisheria zitachukuliwa kwa watakaofanya hivyo-
-Wankyo Nyigesa, RPC Pwani



from MPEKUZI

Comments