Watu 17 wauawa katika shambulizi la kuvizia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Watu zaidi ya 17 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika shambuliolililotokea katika Hifadhi ya Wanyama ya Virunga Kaskazini Mashariki mwa DRC.

Ripoti zinasema kuwa, walinzi 12 wa Mbuga ya Taifa ya Virunga huko mashariki mwa Congo DR, dereva wao na raia wengine 4 wameuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na wanamgambo wenye silaha. Raia wengine wanne wamejeruhiwa.

Yunus Pandasi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa taasisi za kiraia nchini Congo amesema kuwa mauaji hayo yamefanywa na wanamgambo wa Kihutu kutoka Rwanda.

Mbuga ya Taifa ya Virunga iko katika mpaka wa nchi tatu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na Rwanda na imepata umashuhuri wa kimataifa kutokana na kuwa na Sokwe Watu wanaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo hilo la dunia.

-Parstoday


from MPEKUZI

Comments