Marufuku ya Kutotoka Nje Usiku Nchini Kenya Yaongezwa Kwa Siku 21......Wagonjwa wa Corona nchini humo leo Wamefika 343

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya watu kusafiri na kuingia au kutoka katika mji wa Nairobi na miji mingine minne kwa muda wa siku 21 ili kuendelea kukabiliana na Virusi vya Corona

Marufuku ya kutoka nje nyakati za usiku kwa taifa zima pia imeongezwa kwa siku 21.
 
Kenyatta  ametangaza kuwa Kenya sasa ina visa 343 baada ya wengine 7 kuongezeka leo  na wagonjwa waliopona ni 94


from MPEKUZI

Comments