Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa Kukutana na Watengenezaji wa GONGO ili Kuona Namna ya Kuiboresha

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema bado nia yake ya kukutana na Watengenezaji wa pombe aina ya gongo iko palepale

Amesema, lengo ni kujadiliana na kuona namna nzuri ya kuiboresha pombe hiyo kwa kuipelekea TBS na kwa Mkemia ili ipimwe na kuondoa sumu

Amesema, badala ya kuikuza na kuona kuwa hapa kuna kitu kinaweza kutupeleka kwenye viwanda, tunazuia. Je, mnaokunywa hizo pombe za viwandani mnajua asili yake?

Amehoji, "Kwanini gongo haitambuliwi kama kinywaji halisi cha Kitanzania?" Na kusisitiza kuwa atakutana na Watengenezaji wa gongo ili waone namna ya kuiboresha

Amesema “Nasisitiza nitakutana na watengenezaji wa gongo, kama unamfahamu mwambie aje tuzungumze jinsi ya kuiboresha zaidi na ituletee faida, hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda ya zuiazuia, tunapaswa kuwa na Tanzania ya Viwanda ya wezeshawezesha"

Itakumbukwa kuwa Katika Mkutano wa 11, Kikao cha 4 cha Bunge la Aprili 11, 2008, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge alisema yawezekana kabisa tuna pombe kali zaidi ya gongo, la msingi lililozingatiwa katika kupiga marufuku pombe aina ya gongo ni kwa sababu njia inayotumika kutengenezea si ambayo inazingatia usafi na afya ya binadamu, ndiyo maana imekuwa ni haramu kwa mujibu wa sheria.

Pale ambapo viwanda vya kutengeneza pombe ambayo inakubalika kwa masharti ya afya ya binafamu, vitakapoanza kutengeneza gongo, ndiyo hapo ambapo tutazingatia kuihalalisha pombe hiyo.


from MPEKUZI

Comments