Wimbo wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki Kuanza Kuimbwa Rasmi Bungeni na Kwaya Ya Bunge

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kikundi Cha Kwaya  Ya Bunge kimeaanza Rasmi Kuongoza  Kuimba Wimbo Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki Na Wimbo Wa Taifa Pindi  Shughuli Za Bunge Zinapoanza.

Awali, wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi na ufungaji wa mikutano ya Bunge ulikuwa ukiimbwa na kwaya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini leo uliimbwa na watumishi wa Bunge.

Akizungumza leo Jan,28,2020, bungeni jijini Dodoma Spika  Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema mamlaka aliyonayo  kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia sasa bunge ameliamuru kuwa na desturi ya kuimba nyimbo hizo muhimu pindi  vikao na shughuli za bunge zinapoanza .

Ndugai amelishukuru Jeshi la Polisi  kwa kuwafundisha watumishi hao ambapo baada ya kuimba wabunge waliwapigia makofi kuwapongeza. 
___________________

WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


1. Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.

Chorus 

Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.

2. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.

Chorus 

Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.

3. Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.

Chorus 

Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.


from MPEKUZI

Comments