Picha ya Rais Magufuli yamponza Idris Sultan ....Makonda Amtaka Ajisalimishe Polisi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amemtaka mchekeshaji na muigizaji hapa nchini, Idris Sultan, kuripoti katika kituo chochote cha polisi, hii ni baada ya msanii huyo ku 'post' picha katika ukurasa wake wa Instagram, akiwa amehariri picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuweka sura yake.

Makonda ametoa agizo hilo leo Oktoba 30, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagramu.

"Naona mipaka ya kazi yako huijui, nenda sasa hivi kituo chochote cha Polisi, uwaambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako" ameandika Makonda.

Idris aliweka picha hizo ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Rais Magufuli, atimize umri wa miaka 60, ambapo msanii huyo aliandika kuwa.

 "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani".


from MPEKUZI

Comments