Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ahudhuria Mkutano Wa Mawaziri Wa AU Mjini Addis Ababa

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega yuko nchini Ethiopia ambapo anahudhuria mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo, mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.

Mkutano huo ulioitishwa na Kamisheni ya Afrika kupitia Shirika lake la kusimamia Maendeleo ya Rasilimali za Wanyama Barani Afrika (AU-IBAR), unafanyika kwa siku mbili mjini Addis Ababa ambapo mbali na mambo mengine mkutano huo utapokea ripoti na maazimio mbalimbali kutoka kwa wataalam wa sekta hizo kujadili na kuyapitisha ili waweze kupeleka Halmadhauri Kuu ya AU kwa maamuzi na utekezaji.

Moja ya mikakati, ripoti na maazimio na mapendekezo yanayotarajiwa kujadiliwa na kuridhiwa na baraza hilo la mawaziri wa AU wa sekta ya mifugo, uvuvi, kilimo, mazingira na maji ni ripoti ya miaka miwili ya Tathmni ya Azimio la Malabo (Malabo Declaration) lenye lengo la kuondoa njaa katika bara ka Afrika ifikapo Mwaka 2025 na ripoti ya Tathnimi ya kuwasiliana na Majanga ya asili kama mafuriko na ukame.

Maazimio na mapoendekezo mengine ni ripoti ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi, juhudi za nchi wanachama kuzuia matumizi ya bidhaa za plastiki, mkakati wa kupanda mazao yenye viini lishe vya kutosha na mkakati wa kukabiliana na upotevu wa mazao ya mimea na samaki baada ya kufunga (Post harvest Loss).

Katika kikao hicho pia kitajadili mkakati wa kupambana na magonjwa na vimelea sugu kwa mifugo, mpango wa kuanzisha maabara za kupima ubora wa chakula katika bara la Afrika, mpango wa pamoja wa kuwa na kusimamia na kuweza katika wazo la uchumi wa bahari (Blue economy), mpango mkakati wa miaka 10 kuendeleza uvuvi mdogo mdogo (small scale fisheries) na mpango mkakati wa miaka 10 wa kuendeleza sekta ya ukuzaji viumbe maji.

Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi Bi. Josefa Correia Sacko Mkuu wa Kamisheni ya Afrika ya Kilimo na maendeleo vijijini, ambapo zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi 49 za bara la Afrika wanahudhuria wakiwepo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kama FAO, WWF, Benki ya Dunia na NEPAD.

Mwisho.


from MPEKUZI

Comments