Mkurugenzi mstaafu wa kampuni ya Katani Limited, Salum Shamte na wenzake 2 Washitakiwa Kwa Makosa Ya Uhujumu Uchumi

Mkurugenzi mstaafu wa kampuni ya Katani Limited, Salum Shamte na wenzake 2 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga na kusomewa mashtaka matatu ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababishia Amcos hasara ya Sh1.1 bilioni.

Shamte amefikishwa mahakamani leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 pamoja na wenzake,  Juma Shamte ambaye ni mkurugenzi wa sasa wa kampuni hiyo na mjumbe wa bodi ya Katani, Fatma Diwani.

Akisoma mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao mbele ya hakimu mkazi Desidery Kamugisha, wakili wa Serikali, Peter Maugo amesema kati ya Januari 2008 na Agosti 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga na Mkoa wa Tanga, walikula njama kutekeleza mpango wa uhalifu.

Maugo aliyekuwa pamoja na wakili wa Takukuru, Barry Galinoma  na Winlucky Mangowi wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali,  amesema shtaka la pili ni kusababisha hasara katika vyama vitano vya Amcos kiasi cha Sh1.14.bilioni  na shtaka la tatu ni utakatishaji fedha wa Sh1.14 bilioni.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo waliitakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Mawakili wa Serikali wamesema upelelezi wa kesi hiyo iliyoahirishwa hadi Novemba 13, 2019 haujakamilika, washtakiwa kurudishwa rumande.


from MPEKUZI

Comments