Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya Linawashikilia Watuhumiwa Kumi [10] Kwa Tuhuma Mbalimbali.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na Opresheni, Misako na Doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kuhakikisha usalama wa raia na mali unakuwepo ikiwa ni pamoja na wananchi kuendelea na shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato. Oktoba 30, 2019 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendesha Operesheni maalum katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kama ifuatavyo:-

KUPATIKANA POMBE MOSHI @ GONGO.
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha Kibisi, Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi waliwakamata 1. AMBOKILE MWAISABILA [38], 2. ISAYA CHRISTOPHER [28] na 3. ZAINA KASIM [26] wote wakazi wa Kibisi wakiwa na Pombe Moshi @ Gongo ujazo wa lita kumi na mbili [12]. Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa Pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO.
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 11:50 asubuhi huko katika Kitongoji na Kijiji cha Itete – Ndembo, Kata ya Kabula, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Askari Polisi walimkamata TUNU KIJUMILE [21] mkazi wa Ndembo akiwa anauza pombe haramu [gongo] ujazo wa lita tatu [03] Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa gongo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO.
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Igawa, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni maalum walimkamata DAMIN MPINGA [71], mbena, mkulima, mkazi wa igawa akiwa na gongo ujazo wa lita 10 katika chupa 20 ];] mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO.
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Kitongoji cha Matundasi "A" Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.

Askari Polisi wakiwa katika operesheni maalum walimkamata MARIAM SIPO [42] mkazi wa Matundasi "A" akiwa na gongo ujazo wa lita tisa [9] kwenye madumu mawili madogo. Mtuhumiwa ni mpikaji, muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 11:00 asubuhi huko Kijiji cha Kasumulu, Kata ya Ngana, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni walimkamata ABRAHAMU NASON [27] mkazi wa Kasumulu akiwa na bhangi uzito wa kilogram 23 akiwa amehifadhi katika mifuko miwili [2] ya sandarusi na kuificha nyumbani kwake. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 12:30 mchana huko Kijiji na Kata ya Bitimanyanga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori [K.D.U – Iringa] waliwakamata watuhumiwa watatu ambao ni:-

1. ZEPHANIA FURAHISHA [65],
2. ALFRED MWANOGILE [42] na
3. ZAKAYO JACKSON [30] wote wakazi wa Bitimanyanga Wilayani Chunya wakiwa na vipande tisa vya nyama pori idhaniwayo kuwa nyama ya nyati. Watuhumiwa ni majangili.

Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani mara tu upelelezi wa mashauri yao utakapokamilika.


from MPEKUZI

Comments