Ndugai Akerwa na Kiongozi wa Serikali Aliyesema Mbele ya Rais Kuwa Wabunge Wamewadhihaki Wachezaji wa Taifa Stars

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kiongozi mmoja wa Serikali aliyezungumza maneno yasiyofaa kuhusu Bunge la Tanzania na wabunge na kumdanganya hadharani Rais John Magufuli kuwa wawakilishi hao wa wananchi wamewadhihaki wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, hajitambui.

Spika ametoa kauli hiyo bungeni  jana Juni 25, baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, (ACT-Wazalendo), kuomba muongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7), kuhusu jambo lililotokea mapema bungeni.

Zitto alilazimika kuomba muongozo huo baada ya Spika Ndugai kutoa ufafanuzi kwamba hakuna mbunge yeyote aliyewadhihaki wachezaji wa Taifa Stars baada ya mchezo wake na Senegal.

“Mheshimiwa Spika, kwa kutumia kanuni 68 (7), kuhusu jambo lililotokea bungeni mapema, umeelezea jambo ambalo limetokea nje ya bunge kuwa mmoja ya viongozi wa serikali kuwabagaza wabunge waliokwenda Misri.

Mara baada ya mbunge huyo kuomba muongozo huo, Spika Ndugai, alijibu akisisitiza kuwaomba wabunge kutolikuza jambo hilo.

“Naomba tusilikuze jambo hili kabisa, kama wabunge tungekuwa na mawazo kama wachezaji wanamakosa isingewezekana wabunge wengine 30 kwenda Misri. Ni bahati mbaya sana, kwamba tuna viongozi wa serikali, wanadiriki kumdanganya Rais hadharani.

“Kiongozi wa serikali unapoongea mbele ya Rais, jipange, ongea ukweli mtupu mbele ya Mwenyenyezi Mungu na sisi hatutamani kusema, natamani kufunguka kidogo…inatosha..inatosha.

“Nasema wazi bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi kwa sababu ana nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao ambao wanaweza kumtukana Spika, lakini tuache,”alisema.


from MPEKUZI

Comments