Mbunge Ashauri Tozo Ya Pombe ,sigara Ipande Maradufu

Na.Faustine  Gimu Galafoni,
Ikiwa leo Juni 25,2019 Bunge la Tanzania likiwa lina piga kura  ya ndio au hapana ya  kuipitisha au kutoipitisha bajeti kuu ya serikali,wabunge wamekuwa wakitoa michango na maoni mbalimbali kuhusu bajeti hiyo ambapo mbunge wa Rujiji Mohamed  Mchengelwa ameishauri serikali kuongeza tozo kwenye Pombe na sigara . 

Mhe.Mchengelwa amesema kuongeza tozo kwenye pombe na sigara itasaidia kulinda afya za watu kwani watapungua kunywa pombe na sigara kutokana na gharama kubwa  ya  bidhaa hizo ambazo sio muhimu kwa maisha ya binadamu  kwani husababisha madhara kiafya pamoja ,uchumi kudumaa, migogoro kutokana na walevi  kuwa na fujo zisizo za msingi. 

Hivyo Mbunge huyo amesema serikali hutumia gharama kubwa katika matibabu kwa watu walioathirika na utumiaji wa pombe na sigara Mfano,TB, ili kupunguza gharama hizo na kuepusha madhara kwa watanzania ni wakati sasa umefika tozo  za pombe na Sigara zikawa kubwa maradufu. 

Katika hatua nyingine mbunge huyo ameishauri serikali kufanya tathmini ya Madhara ya Ukoloni  uliotokea na kubainisha hasara na madhara ya ukoloni ili Tanzania ifungue kesi ya kimataifa dhidi ya nchini zilizokuwa makoloni ya Tanzania ambazo ni Ujerumani na Uingereza ili ziweze kuipa fidia Tanzania kwani baadhi ya nchi za Afrika zilishawahi kufanya hivyo na kulipwa. 

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya miezi ya hivi  karibuni kuona clip ya video   ya  Bunge la Ujerumani ikishinikiza Taifa la Tanzania kusitisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa  mto Rufiji wa Stieglers Gorge   wakidai kuwa wao ni koloni la Tanzania. 

Ikumbukwe kuwa mradi wa umeme wa Mto Rufiji Stieglers Gorge unagharimu  dola za kimarekani Bilioni 2.9  na ukikamilika utazalisha Megawati 2,100 na hatua hiyo ya utekelezaji  imekuja baada ya miaka 40  ya utafiti.


from MPEKUZI

Comments