Madini ya Mamilioni ya Pesa Yakamatwa Yakitoroshwa Kuelekea Kenya

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata madini aina mbalimbali ambayo  yalikuwa yakitoroshwa kuelekea nchi jirani ya Kenya.


Madini hayo zaidi ya kilo 36 yamekamatwa jana Jumatano Juni 26, 2019 na askari maalum ya intelijensia baada ya kupata taarifa madini hayo kutoroshwa kutoka Arusha katika basi la Perfect trans ambalo hufanya safari kutoka Arusha hadi Nairobi nchini Kenya.

Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema madini hayo ikiwepo Tanzanite kilo tano, Ruby na Greentonaline  yalikuwa yanasafirishwa kwenye mfuko mkubwa yakiwa yamechanganywa na mchele.

Amesema dereva wa gari hilo na kondakta wake wanashikiliwa kwa mahojiano wakidai hawamjui mmiliki wa madini hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank James Mwaisumbe akishuhudia madini zaidi ya kg 36 zikiwemo 24 za Tanzanite yenye thamani ya mabilioni yaliyokamatwa hapo jana mpakani Namanga yakivushwa kwenda Kenya na dereva na kondakta wa basi la abiria la Perfect.


from MPEKUZI

Comments