Baadhi ya Wabunge Kenya wamuunga mkono Jaguar....Wataka aachiwe huru

Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles 'Jaguar' Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wakiwemo watanzania  wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa jana  mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa.

Baadhi ya wabunge nchini humo  wakichangia mjadala huo wameunga mkono kauli ya Jaguar huku wakitaka aachiwe huru kwani alichosema ndio mtazamo wa Wakenya waliowengi.

Akichangia maoni bungeni jana Juni 26, 2019, Mbunge wa Garissa mjini, Aden Duale amesema Jaguar alifanya jambo la kizalendo kwani Taifa hilo linahitaji kuwalinda wananchi wao kwenye masuala ya kibiashara.

Mbunge mwingine ni Moses Kuria wa jimbo la Gatundu Kusini, Amesema kuwa kauli ya Jaguar sio ngeni kwani viongozi wengi wa nchi hiyo walishawahi kuongea kuhusu wageni kupora fursa za kibiashara nchini humo.

Jana Mbunge wa jimbo la Starehe, Jaguar alishikwa na maafisa polisi katika viunga vya bunge la nchi hiyo na mpaka sasa bado hajaachiwa.

==>.Wasikilize hapo chini


from MPEKUZI

Comments