Waliokuwa Wafanyakazi Bandari Kavu ya Azam ICD Watupwa Jela Miaka Mitatu

Mahakama Kuu divisheni ya Rushwa na uhujumu uchumi imewahakumu wafanyakazi wawili wa zamani wa bandari kavu ya Azam ICD kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bil.12.7 na kuachiwa kwa makosa ya kutakatisha fedha na kukwepa kodi.

Pia mahakama imemuhukumu Benson Malembo mfanyakazi wa Region Cargo Service kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh. Bilioni 12.

Mbali na Malembo, washtakiwa waliotiwa hatiani na kusomewa Hukumu yao  leo Machi 28.2019 na Jaji Winifrida. Korosso ni Raymond Adolf Louis ambaye ni Meneja wa oparesheni za usalama na  Khalid Yusufu Louis.

Louis na Hassan wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kila mmoja kwa kila shtaka katika mashtaka 104 ya kughushi na kifungo cha miaka miwili kila mmoja katika shtaka moja la kuisababishia Mamlaka ya Mapato (TRA) hasara ya Sh12.5 bilioni.

Akitoa adhabu hiyo, Jaji Korosso amesema adhabu zote hizo zinakwenda kwa pamoja.

Mbali na adhabu hiyo ya kifungo, pia Jaji Korosso ameamuru washtakiwa baada ya kumaliza kifungo chao kuilipa TRA fidia ya nusu ya hasara waliyoisababishia, yaani zaidi ya Sh6 bilioni wote kwa pamoja.

Malembo amehukumiwa kutumia adhabu ya miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika shtaka moja la kuisababishia TRA hasara hiyo ya Sh12.5 bilioni.

Upande wa mashtaka uliita jumla ya mashahidi 34 mahakamani hapo  kutoa ushahidi wao ambapo Jaji Korosso amesema  kupitia ushahidi huo, upande wa mashtaka umethibitisha kesi dhidi ya washtakiwa hao.

Hata hivyo, mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa  waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo  baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Washtakiwa walioachiwa ni, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary, Haroun Mpande wa kitengo cha mawasiliano na kompyuta ICT TRA


from MPEKUZI

Comments