Taarifa Kwa Umma Kuhusu Uhakiki Wa Vibali Vyote Vya Taka Hatarishi

Ofisi ya Makamu wa Rais imepewa mamlaka ya kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu mazingira nchini kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, 2004 na Kanuni zake. 

Aidha, usimamizi na udhibiti wa taka zenye madhara umebainishwa kwenye Vifungu vya 133 -139 vya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004. Pia Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Usimamizi na Udhibiti wa Taka za Hatarishi) za Mwaka 2009 zimetoa miongozo ya kudhibiti taka hatarishi hapa nchini pamoja na mambo mengine yahusuyo uhifadhi wa mazingira.

Kwa muktadha huo, Ofisi ya Makamu wa Rais inawaagiza watu wote wenye leseni za kukusanya taka hatarishi ikiwemo Vyuma Chakavu, Betri zilizotumika na Taka za Kielektroniki kuwa, wapeleke leseni zao halisi (Original Certificates) katika Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) zilizopo karibu yao kwa ajili ya uhakiki. Leseni ambazo hazitahakikiwa kufikia tarehe 02/04/2019 zitakuwa Zimefutwa.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inatoa wito kwa wananchi wote kuwa mtu yeyote atakayejihusisha na ununuaji au uuzaji wa vyuma chakavu vinavyotokana na miundombinu ya taifa atashitakiwa kwa kosa la uharibifu wa miundombinu chini ya sheria za uhujumu uchumi.

Mhandisi Joseph Malongo
KATIBU MKUU

 25 MACHI 2019
 


from MPEKUZI

Comments