Rais Magufuli awajibu walioomba mapumziko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kwamba watanzania jana walifurahi sana baada ya ushidi ndiyo maana walitaka kupewa siku ya leo iwe ya mapumziko.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipokutana na wachezaji wa timu ya taifa Ikulu pamoja na bondia Hassan Mwakinyo.

Amesema hakushangazwa baada ya kuona kwenye mitandao ya kijamii watu wakisema kwanini asitangaze leo iwe siku ya mapumziko.

"Wengine walikuwa wanasema kwanini usitangaze kesho ikawa mapumziko, nikasema watanzania na mapumziko jamani. Ila sikushangaa ndiyo dhana ya kusfurahi."

Amesema hakushangazwa kuona watu wamelewa kwa kuwa anaamini ilikuwa ni furaha kwani hata watu wengine hawakwenda majumbani kwa madai bado walikuwa wanashangilia.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewajulisha Taifa Stars, kwamba watanzania wanapenda furaha wakati husika hivyo jana walifanikiwa na wanapaswa kufanya hivyo kwenye michezo mingine.

Timu ya Taifa ya Tanzania imefuzu kushiriki michuiano ya mataifa ya AFCON 2019 ambapo Tanzania imeungana na nchi zingine kutoka Afrika Mashariki, Kenya, Uganda na Burundi.


from MPEKUZI

Comments