Jeshi La Polisi Lazuia Mkutano wa ACT-Wazalendo

Jeshi la Polisi Tanzania wamezuia Mkutano wa ACT-Wazalendo kwa sababu ya kuhofia wafuasi wa CUF chini ya Profesa Lipumba kuvuruga mkutano huo. 

Mkutano huo wa ndani ulipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PR Stadium uliopo karibu na Uwanja wa Taifa.

Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo leo March 27,2019  wakiongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe, Maalim Seif, Naibu Kiongozi wa Chama, Duni Haji walikuwa wakitarajia kukutana na wanachama wa ACT - Wazalendo.

Viongozi wengine ambao walitarajiwa kuwa kwenye mkutano huo ni pamoja na  Mwenyekiti wa chama Ndugu Yeremia Maganja, Makamo Mwenyekiti Bara Ndugu Shaaban Mambo, Katibu Mkuu, Dorothy Semu na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mtemelwa pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dar es salaam.


from MPEKUZI

Comments