Waziri Kigwangala Ateua Wajumbe Wa Bodi Ya Wakurugenzi Ya Mamlaka Ya Usimamizi Wa Wanyamapori Tanzania – (Tawa)

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb.), amekamilisha uteuzi wa safu ya wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – (TAWA), kulingana na mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3.1.1 cha amri ya uanzishwaji wa Mamlaka ya TAWA ( GN na. 135 ya mwaka 2014)  kwa kuwateua wajumbe wengine wawili.
 
Wajumbe walioteuliwa kukamilisha safu inayotakiwa ni;
(i)    Bi. Jane Claude Mihanji  na
(ii)    Bi Magdalena Joseph Kimaty
 
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2018.
 
Wakati huo huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, amebatilisha uteuzi wa Dkt. Freddy S. Manongi kuwa mjumbe wa bodi ya TAWA.

Imetolewa na

Dorina G. Makaya
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
27 Februari, 2019


from MPEKUZI

Comments