Mdhibiti mkuu wa Ubora wa Elimu Kanda kati ,Bw.Sospeter Magina Jana Februari 19,2019 amefanya kikao na wamiliki wa Taasisi binafsi za Elimu mkoani Dodoma na kujadili Masuala mbalimbali ya kielimu ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuzingatia maadili katika taasisi zao.
Akizungumza Katika kikao hicho kilichofanyika shule ya sekondari Dodoma ambacho kimekutanisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo maafisa elimu msingi na sekondari jiji la Dodoma,Bw.Magina alisema suala la maadili ni la tangu zamani hivyo ni vyema kila Shule ikazingatia kusimamia maadili ya wanafunzi na walimu.
“Suala la maadili halijawahi kubadilika tangu nyaraka za miaka iliyopita tatizo ni usimamizi wa nyaraka hizo kuhusiana maadili ya wanafunzi na walimu sio mzuri hivyo mnatakiwa kuzingatia kusimamia maadili ipasavyo”
Aidha ,Bw.Magina alizungumzia juu ya suala la ufundishaji shuleni kwa kuzingatia Mtaala wa elimu uliopo wakati mchakato wa vitabu ukiandaliwa .
“Suala la mitaala ieleweke wazi kuwa kulikuwa na shida ya vitabu fulani vilivyokuwa vinaingia mashuleni ,serikali imechukua jitihada kuhakikisha ya kwamba vitabu vipya vinaandaliwa .Taarifa nilizonazo kwa sasa karibu vinatoka ,muda wowote vinatoka .Walimu wanatakiwa kufundisha kwa kuzingatia syllabus wakati vitabu vipya vikiandaliwa.”
Hata hivyo Mdhibiti huyo wa ubora wa elimu kanda ya kati Dodoma alisema kuwa haiingii akilini shule za Dodoma haziingii kwenye kumi bora kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa hivyo kuna haja ya kufanya mabadiliko sasa ili mkoa huo ujipambanue vyema na kufanya vizuri katika masuala ya kielimu.
MWISHO.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment