Waziri Kairuki Akutana Na Watumishi Wa Ofisi Ya Waziri Mkuu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na watumishi wa ofisi yake kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli kushika wadhifa huo mpya.

Waziri Kairuki amekutana na watumishi hao mapema hii leo (Januari 30, 2019) katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma na kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kujua ofisi hiyo.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde pamoja na Makatibu wakuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu pamoja na Dorothy Mwaluko anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji.

Kairuki waliwataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa umoja na uzalendo ili kujilete maendeleo nchini na kuahidi kushirikiano nao kwa kipindi chote atakachokuwa katika Ofisi hiyo.

“Kipekee ninawashukuru viongozi na watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mapokezi mazuri na  hii ni ishara ya umoja wenu na ninaahidi kushirikiana na watendaji wote katika utekelezaji wa majukumu tuliyonayo  kwa maslahii mapana ya ofisi yetu na Taifa kwa ujumla,”alisisitiza Kairuki

Naye Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo Mhe.Jenista Mhagama alipongeza watumishi wa Ofisi yake kwa kuendelea kutekeleza majukumu na kuwataka kuwa na uzalendo na weledi wa hali ya juu.

“Ninachoweza kusema tutaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa kazi za kila siku kwa kuzingatia kuwa hii ni familia moja yenye nia moja ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais ili kujiletea maendeleo katika nchi yetu,”alisema Mhagama.


from MPEKUZI

Comments