Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Yaomba Radhi Kivuko cha MV. MAGOGONI Kuharibika

Leo tarehe 09/01/2019 mnamo saa 1:30 asubuhi kivuko cha MV. MAGOGONI kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kilipigwa na upepo mkali wakati kikikaribia upande wa Kigamboni. 

Hivyo, katika hali ya kupambana na upepo mitambo ya kuendeshea kivuko hicho iliingiliwa na takataka ambazo zilisababisha injini kupata moto na kupata hitilafu. 

Mafundi wetu wamefanikiwa kutatua hitilafu hiyo na huduma za kivuko hicho zimerejea katika hali ya kawaida mnamo saa 6:30 mchana. 

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unawaomba radhi abiria wote kwa usumbufu walioupata.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
TEMESA
09/01/2019


from MPEKUZI

Comments