Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 56

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
Nikagonga kidogo na ukafunguliwa. Biyanka akanipokea kwa sura iliyo jaa hasira sana, sikuhitaji kusemeshea kitu cha aina yoyote zaidi ya kuingia ndani. Nikavua koti langu na kulirusha kwenye kiti.
“Umetoka wapi na ulikuwa wapi na ulikuwa na unafanyaje na kwa nini ulinikatia simu kisha ukazima eheeee?”
Biyanka alizungumza kwa ukali sana ambao sikuujali, nikaka kwenye sofa na kuweka nne, nikailegeze vizuri tai yangu kisha nikapitia meseji za afande Kimaro. Nikajikuta nikinyanyuka huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana mara baada ya kusoma meseji ya Afande Kimaro akidai kwamba Clara haonekani hospitalini na askari wake wawili alio kuwa amewaacha waimarishe ulinzi wameuwawa usiku wa kuamkia leo.

ENDELEA
Sikutaka kuendelea kujishauri kichwani mwangu kwa muda mrefu, nikaitafuta namba ya afande Kimaro na kumpigia, ikaanza kuita kwa muda kisha ikapokelewa.
“Ndio, afande”   
“Nimejaribu kukupigia simu yako kwa muda kidogo nikaona kimya”
“Ni kweli afande nilizima ili watu wale walio panga kuniaua wasiweze kunitafuta kwa kupitia simu yangu”
Biyanka akastuka macho yakamtoka, kwa haraka akanisogelea sehehemu nilipo simama. Uso wa hasira ambao ulikuwa umumtawala nikaushuhudia taratibu ukianza kumuondoka na kuwa mpole huku akinisikiliza kwa umakini kile nilicho kizungumza.
 
“Ahaa sawa sawa nina imani kwamba meseji zangu umewezeza kuziona?”
“Ndio nimeweza kuzioana kwa sasa mupo wapi?”
“Nipo kituaoni, unaweza kufika”
“Sawa ninakuja sasa hivi”
Nikakata simu na kuirudisha mfukoni.
“Ethan nitakuwa nimesikia vibaya, umesema kwamba kuna watu walihitaji kukuaa?”
“Ndio”
 
Nikaitafuta meseji ya vitisho niliyo tumiwa na nikamkabidhi Biyanka simu yangu kisha mimi nikaelekea bafuni kuweza kunawa ili niweze kutoa harufu harufu ya pafyumu za Qeen na Latifa. Nikatoka bafuni na kumkuta Biyakna akizungumza na simu.
“Ehee baba wanamtishia mume wangu anahitaji kumuua”
Nikataka kumzuia Biyanka asizungumze na baba yake juu ya hili swala ila nikajikuta nikiwa nimesha chelewa kumzuia.
“Ndio nimekutumia, tayari hiyo namba. Hembu  baba nakuomba basi watu wako wa usalama wamtuafute muhisika wa hili tukioa basi”
“Mume wangu anaogopa amekuwa ni mtu wa kuzima zima simu kila mara jamani”
 
Biyanka alizungumza kwa masikitiko makubwa akionekana ameguswa sana na hili swala.
“Ndio yupo hapa”
“Eheee”
Biyanka akanikabidhi simu yake nikaiweka sikioni.
“Shikamoo baba”
“Marahaba. Ethan una ugomvi na mtu wa aina yoyote?”
“Hapana baba yangu, Tanzania mimi sina hata rafiki kabisa, na nimeshangaa mtu huyo ni wapi  ameipatia namba yangu na kwa nini ananitisha ikiwa sijafanya jambo lolote baya”
“Punguza wasiwasi, swala lako  nitalihushulikia mwanagu sawa”
“Sawa baba yaani nimejikuta ninanunua gari jipya ili wasiweze kunikremisha kwamba ni mimi”
“Hahaaa, hivi huna mlinzi”
“Ndio kwa sasa sina mlinzi”
“Basi nitaagiza vijana wangu wawili wawe wanakulinda kila unapo kwenda. Nina imani wana ujuzi mkubwa sana wa kukufanya uwe salama kila muda”
“Nashukuru sana baba yangu”
 
“Sawa sawa, niwatakie mchana mwema na nitawajulisha mara baada ya kuweza kumkamata muhusika wa hili tukio”
“Sawa baba”
Nilijikaza kumuita tu baba, ila laiti kama angefahamu kwamba yeye ndio adui yangu namba moja basi asinge weza kujipendekeza sana kwangu. Simu ikakatwa, Biyanka kwa haraka akanikumbatia huku akilia.
“Jamani pole mume wangu, nilihisi kwamba unanisaliti jamani”
“Siwezi kukusaliti mke wangu, kwa nini nifanye hivyo ikiwa nina kupenda kuliko kitu chochote.”
“Nisamehe kwa kuweza kukufikiria vibaya mpenzi wangu. Nisamehe kwa kweli”
“Usijali mpenzi wangu. Nahitaji kuelekea polisi kwa sasa, tunaweza kuongozana?”
“Ndio”
 
“Nitolee nguo hapo kabatini”
Biyanka akaniachia na kufanya nilicho muagiza. Nikavaa nguo hizi huku nikijaribu na mimi kuweza kuumiza kichwa juu ya baba mdogo wa Clara tuliye mkamata ana kundi kubwa kiasi gani la kuweza kufanya mauaji ya kiasi hichi kisa kikubwa ni Clara.
“Usiwe na mawazo sana mume wangu, kila jambo litakuwa sawa”
Biyanka alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu. Tulipa maliza kujiandaa tukatoka ndani humu na kuelekea eneo la maegesho. Tukaingia kwenye gari langu hili jipya.
“Gari nzuri”
Biyanka alizungumza huku akilichunguza gari langu kwa ndani.
 
“Nashukuru, walinzi wako wapo wapi?”
“Gari zao zile pale”
Tukaanza kuondoka eneo hili taratibu huku gari za walinzi wa Biyanka zikitufwata kwa nyuma. Tukafika kituo kikuu cha polisi na moja kwa moja tukaelekea ofisini kwa afande Kimaro. Akatukaribisha kwa furaha kiasi huku wakionekana kufahamiana sana Biyanka.
“Ila baba anaendelea vizuri”
“Ndio anaendelea vizuri na nilisha mdokezea juu ya lile ombi lako la kuwa IGP”
“Akasemaje?”
“Kama kawaida yake, subiri nipate Ikulu mwanangu kila jambo litakwenda sawa”
 
Biyanka alizungumza huku akiwa ameiigiza sauti ya baba yake jambo lililo tufanya sote tucheke.
“Kumbe muna fahamiana na Ethan?”
“Ndio ni mume wangu mtarajiwa”
“Weee kumbe ningemkoromea mwanzoni nahisi hata hii nafasi ningepokonywa”
“Haaaa ndio”
“Nashukuru Mungu damu zetu mimi na Ethan zimeendana”
“Nanyi mumejuana vipi?”
“Ni swala la binti mdogo aliye muokoata nina imani kwamba atakuwa amekusimulia?”
“Binti gani mume wangu?”
 
“Yule niliye kuambia kwamba nimemuokota kule kwenye maegesho ya magari pale ofisini”
“Ahaaa…ehee amefikia wapi?”
Afande Kimaro akafungua faili moja na kulisogeza karibu yetu. Tukaona picha za askari walio uwawa katika mlango wa chumba ambacho alilazwa Clara.
“Muuaji ni mwanamke, sura bado hatujaweza kuifahamu na alivalia mavazi ya kidaktari na aliweza kuifumba sura yake kwa kutumia vile vitambaa vyoa wakiwa katika chumba cha upasuaji”
Afande Kimaro alizungumza huku akituonyesha picha za msichana huyo ambazo imerekodiwa na CCTV kamera. 
 
“Baada ya kufanya mauaji ya vijana wetu wawili, akaingia ndani na kumchukua mtoto nahisi alimchoma sindano ya usingizi, alimpakiza kwenye kiti kile cha magurudumu nakuanza kumsukuma kumpeleka nje na aliweza kuzi vunja kamera za nje ambazo hatukuweza kujua aliondoka pale hospitalini kwa gari gani”
 
“Ila pale hospitalini niliweza kumuona mlinzi naye hakuona jambo lolote?”
“Mlinzi hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo. Ila vijana wangu wanaendelea na msako mkali sana na watahakikisha kwamba wanamtia nguvuni msichana huyo”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikionekana kuchoka sana.
“Je muhusika wa namba ambaye amenipa vitisho vipi?”
“Yule muhisika bado tunaendelea kuitafuta namba yake kwenye mitandao ila bado hatujampata”
“Basi utanifahamisha kile ambacho kitaendelea”
“Sawa Ethan”
 
“Kimaro, jitahidini basi, mume wangu mumemfanya aishi maisha ya woga ikiwa yupo Tanzania nchi yenye amani kuliko nchi zote Afrika bwana”
“Usijali nitahakikisha hili swala linakwenda kuwa sawa hivi karibuni”
“Sawa tunashukuru”
Tukaagana na afande Kimaro na kutoka ofisini humu. Tukaingia kwenye gari letu huku kichwa changu kikiwa na msongamano wa mawazo.
“Utaweza kuendesha kweli mume wangu?”
Nikamjibu Biyanka kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba sinto weza kuendesha gari hili. Nikampisha Biyanka kwenye siti ya dereva na tukaondoka eneo hili la kituo kikuu cha polisi cha kati.
 
“Kichwa chako mume wangu hakipo sawa, unahitaji tuelekee wapi kupata mapumziko”
“Nahitaji kwenda kulala sasa hivi”
“Huitaji kukaa labda kwenye sehemu ukapunga upepo wa bahari hivi”
“Nahitaji kulala, watu wananiwinda. Unataka wakaniulie huko baharini ehee?”
Nilizungumza kwa ukali kidogo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Biyanka akajawa na unyonge ulio mfanya ajikute akiomba msamaha pasipo kunifanyia jambo lolote baya. Tukafika hotelini na kuingia chumbani kwetu.
“Ethan naona ni vyema nikakuacha peke yako upumzike, ninaelekea nyumbani nitarudi usiku”
 
“Sawa”
Biyanka akanitazama kwa muda kidogo kisha akanisogelea na kunibusu mdomoni mwangu.
“Ninakupenda sana mume wangu”
“Ninakupenda pia mke wangu”
“Kweli?”
“Ndio au unahisi kwamba nina kudanganya?”
“Hapana mume wangu, nashukuru kwa kunipenda”
“Poa”
Nikajitupa kitandani, Biyanka akanitazama kwa unonge sana kisha akanivua viatu, akaviweka sehemu yake, akataka kunivua suruali ila nikamzuia kwa ishara.
“Nenda tu nyumbani”
“Sawa mume wangu”
Biyanka akanibusu shavuni kisha akatoka ndani humu. Nikanyanyuka kwa haraka hadi mlangoni, nikaufunga vizuri kwa komeo, kisha nikaitoa simu yangu mfukoni na kumtafuta Camila nina imani kwamba atakuwa amenitafuta. Simu ya Camila ikaanza kuita, kisha aikapokelewa.
“Niambie mume wangu”
“Poa baby vipi?”
“Safi, leo nimehitimu mafunzo yangu ya juto, kung fu na taikondo”
 
“Umeyasomea wapi hayo mafunzo”
“Si Dany amenifundisha, yaani hapa nipo vizuri sana. Mtu anizingui kabisa”
“Hahaa kama ninakuona vile”
“Weee yaani, siku nikikufuamania na mwanamke, yaani nitampiga hadi ajute kuzaliwa”
Tabasamu nililo kuwa nalo usoni mwangu, likapotea gafla kwani hiyo ni si taarifa nzuri kwani huku nilipo nimesha tambulishwa kabisa.
“Sawa mama”
“Mbona unanijibu kwa unyonge”
“Hamna, mwenzangu sasa hivi upo vizuri, mimi bado”
“Nitakufundisha. Uzuri wa mke wako kichwa changu kina shika mambo kwa haraka na ninaweza kumsaidia hata mtu mwengine katika swala zima la kumfundisha”
 
“Sawa, ehee niambie”
“Kesho ninaanza mazoezi mawili ya mwisho, moja ni kutumia upanga na na jengine kutumia silaha”
“Mmm angalia asije kufundisha ugaidi bure”
“Hahaaa hii ni kwaajili ya kujilinda na familia yetu. Natambua baba wewe una mambo mengi kwa namna moja ama nyingine mimi mama nitasimama kama mlinzi wako”
“Hahaa, haya bwana mama watoto”
“Nikimaliza, tunarudi Ujerumani, ume umemaliza, hujamaliza tunarudi Ujerumani. Mama yangu amenimiss sana”
“Sawa mpenzi wangu, wanaendeleaje lakini?
 
“Wanaendelea vizuri”
“Nashukuru kusikia hivyo”
“Fanya uwasiliane nao”
“Poa mpenzi wangu”
“Haya baadae, tambua nina kupenda na kukuhitaji. Mtu akijichanganya kwako nami ninamchanganya kisawa sawa”
“Hahaa haya bwana mama”
Nikakata simu, nikaitafuta namba ya mtu ambaye amenitumia meseji ya vitisho, nikampigia ila kwa bahati mbaya nikakuta kwamba hapatikani hewani. Gafla nikamuona Ethan akiwa amekaa kwenye moja ya sofa huku akiwa amevalia suti nyeupe na inayo ng’ara vizuri.
 
“Naona unaumiza kichwa sana kwa mtu aliye kukoromea?”
“Wewe unahisi nitakuwa na furaha jaaa yangu”
“Hhaaa….hawawezi kukuua”
“Wewe umesha mfahamu mtu ambaye amenitishia?”
“Ninaweza kumfahamu”
“Ni nani”
“Vaa viatu twende”
Nikavaa viatu na tukatoka katika chumba hichi na Ethan, watu ninao kutana nao njiani hawawezi kumuona Ethana zaidi ya mimi pekee, nikakabidhi kadi ya chumba changu mapokezi na tukaingia kwenye gari. Ethan akaanza kunielekeza hadi kwenye moja ya gorofa moja linalo jenge na halijamaliziwa.
 
“Simamisha gari hapa, tukifika pale mambo yanaweza kuwa mabaya”
“Kwani ni kina nani?”
“Wewe twende”
Nikasimamisha gari kwenye mitimiti kadhaa, tukashuka kwenye gari na Ethan akanisogogelea na kunishika mkono wangu wa kulia na kuniambia kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuniona nikitembea katika eneo hili. Tukapandisha hadi gorofa ya tano, nikaanza kusikia vilio vya mtu akigugumia kulia kwa kipigo anacho kipokea kutoka kwa mtu anaye mpiga. Tukaingia kwenye chumba hicho, sikuamini macho yangu mara baada ya kumkuta baba mkwe, Biyanka pamoja na walinzi wapatao kumi huku Biyanka akimpiga kijana huyo kwa rungu kubwa.
 
“Niliwakanya mucheze na kote ila si kucheza na mume wangu. Kama muna fanya kazi chini ya baba yangu mufanye tu ila si kumgusa mume wangu sawa wewe mwana haramu”
Biyanka alizungumza  huku akihema, akafuta jasho linalo mtiririka usoni mwake, kisha akaandelea kumshushia marungu kijana huyu huku baba yake akitabasamu kwa binti yake kuifanya kazi hiyo ya kikatili sana.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments