Mume wa AMBER RUTTY Adondoka Mahakamani

Msanii na 'video queen' kwenye video za wasanii, Amber Rutty ameeleza sababu iliyopelekea mume wake, Said Mtopali kudondoka ghafla mahakamani kuwa ni kutokana na hali ya kizunguzungu aliyokuwa akijisikia.
 
Amber Rutty amesema kwamba hali ya mume wake haikuwa nzuri tangu walipotoka gereza la Segerea kwa kuwa walikumbwa na maradhi.

Amber Rutty amesema kwamba kwa sasa mume wake ameshapatiwa huduma ya kwanza na tayari amepatiwa 'drip'mbili za maji.

"Hali yake haikuwa nzuri sana tangu tulipotoka magereza. Wote tuliondoka kule na magonjwa, ila yeye alikuwa akiumwa sana. Namshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri", amesema Amber Rutty.

Leo Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Mbando ameahirisha kesi inayowakabili wanandoa hao kwa kusambaza video chafu mitandaoni hadi Februari 11, 2019 baada ya Wakili Neema Mbwana kusema upelelezi haujakamilika.

Wanandoa hao wapya ambao wamefunga ndoa wiki iliyopita wamedai baada ya matatizo yao kwisha watafanya sherehe ili kusherehekea ndoa yao.


from MPEKUZI

Comments