Kikosi Cha IGP Siro Chatua Njombe Kuwasaka Wauaji Wa Watoto

Ikiwa siku moja imepita tangu naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP Siro kutuma kikosi maalumu cha kiintelinsia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na wauaji wilayani Njombe , Hatimae hii  jana kikosi hicho kimewasili mkoani Njombe kikiongozwa na Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini Nsato Marijani.

Akizungumza katika mkutano wa dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Njombe mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka wakati akitamburisha kikosi hicho kilichosheheni wataalamu mbalimbali kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wamaovu hayo huku akidai hakuna mtu atakae achwa salama kama amehusika na mauaji.

Katika mkutano huo pia Olesendeka amemuagiza kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RPC Rennata Mzinga kumkamata mara moja aliyekuwa mratibu wa tiba mbadala na asilia mkoa wa Njombe Matias Gambishi ambaye pia ni afisa afya wa mkoa huo baada ya kulalamikiwa na waganga wataalamu wa tiba asili na mbadala kuwa amekuwa chanzo cha kusababisha migogoro katika chama chao pamoja kufanya usajiri holela wa waganga hao.

Nae kamanda wa kikosi hicho maalumu Nsato Marijani ambaye ni  Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini alisema kikosi hicho kimekuja kwa kazi ya kuwasaka wahusika wa mauaji na kwamba kitawasaka popote walipo kwa heri ama shari.

Kwa upande wananchi wanapongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto.


from MPEKUZI

Comments