Benki Kuu (BoT) yataja sababu mbili kushuka shilingi

Benki Kuu (BoT), imesema kutokuwapo kwa bidhaa za kuuzwa nje ya nchi na pia watalii kupungua katika kipindi cha Januari zinaweza kuwa sababu za kushuka kwa shilingi dhidi ya Dola ya Marekani.

Mkurugenzi wa Uchumi, Utafiti na Sera wa BoT, Suleiman Misango alisema katika mahojiano na gazeti la The Citizen juzi kuwa katika kipindi cha miezi ya Desemba na Januari, shilingi ina kawaida ya kushuka na kupanda kulingana na Dola.

Kiwango cha ubadilishaji fedha za kigeni cha BoT kimeonyesha kuwa hadi juzi mauzo ya shilingi ya Tanzania yalikuwa Sh2,294 na ilinunuliwa kwa Sh2,271 ikilinganishwa na Sh2,249 na Sh2,227 iliyorekodiwa Januari 29, mwaka jana.

Ripoti ya soko la fedha ya ya benki hiyo pia imeonyesha kuwa Dola ilikuwa ikibadilishwa kwa wastani wa Sh2,294 kama ilivyorekodiwa Ijumaa wiki iliyopita, kutoka Sh2,249 iliyobadilishwa Januari 29, mwaka uliopita.

Hata hivyo, Misango alisema kuwa anguko hilo la shilingi linasababishwa na mwezi wa Januari kutokuwa po kwa bidhaa za kuuza nje ya nchi na pia wingi wa watalii.

“Kwa kawaida katika kipindi cha Desemba huwa inapanda lakini ikifika Januari kunakuwa na mahitaji makubwa kwa kuwa mashirika na watu binafsi wanazitafuta ili kukidhi mahitaji yao yanayohusu mwisho wa mwaka,” alisema.

Misango alisema mambo yatakuja kubadilika baada ya watalii kuanza kuongezeka nchini na uuzwaji wa bidhaa za ndani nje ya nchi, na hivyo wataongeza fedha za kigeni.

Credit: Mwananchi


from MPEKUZI

Comments