Mzazi Mwenza wa Msanii Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’’ Afunguka Maneno MAZITO Akijiandaa Kuupokea Mwaka Mpya 2019

Mzazi mwenzie wa msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’’, amesema kuwa yuko tayari kuupokea mwaka 2019, kutokana na miaka miwili 2017 na 2018, alipitia matatizo makubwa ikiwamo la kuondokewa na maama yake mzazi.
 
Kupitia ukurasa wake wa Instagraam, Zari, alisema kuwa mwaka 2017 alipitia katika kipindi kigumu cha koondokewa na Mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake Ivan.

Pia, alieleza namna alivyoutumia mwaka 2018 katika kujemga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia, kujijenga zaidi baada ya kuondokewa na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.
 
“Mwaka 2019, niko tayari kwa mwanzo mpya… Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote  tunajifunza. Asante 2018, bado nina pumua.Asante, Nishirikishe hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018,” aliandia Zari.

“2017 i was shattered in ways i could never explain, 2 major deaths of my loved ones, infidelity and other things. 2018 was all about picking up my broken pieces and rebuilding. 2019 am simply ready for a new beginning….

"In life, we hurt, we make mistakes, we forgive, we move on. But, most of all & through it all we learn. Thank You 2018, i still have my breath. #Grateful #Blessed #Thankful Share with me your life story of 2018….,”
-ZARI



from MPEKUZI

Comments