Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Aonya Kuhusu Rushwa, Lugha Chafu

MKURUGENZI  Mtendaji  wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence  Museru  amesema  uongozi  wa  hospitali  hiyo  utachukua   hatua    za    kinidhamu    mtumishi    atakayejihusisha   na   vitendo   vya   rushwa  na  kutoa  lugha  chafu  kwa  wateja.

Haya    aliyasema    jjini    Dar  es Salaam juzi wakati akifungua mkutano  mkuu  wa  mwaka  wa  Chama  cha Wafanyakazi wa Afya Serikalini (TUGHE), tawi la Muhimbili.
 
Alisema,   kuwa   mtumishi   wa   umma    anapaswa    kuwa    mfano    katika  kutoa  huduma  bora  na  kuzingatia nidhamu.

Prof.   Museru   alisema   endapo   itabainika  kwamba  mtumishi  kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali zitachukuliwa   dhidi   yake   ili   iwe   fundisho kwa wengine.
 
“Jina    la    Muhimbili    liendelee    kuwa  safi  tusikubali  watu  wachache    watukwamishe    ni    lazima    tushirikiane   katika   kuwafichua watu  hao  ili  hatua  stahiki  ziweze  kuchukuliwa   dhidi   yao,”   alisema   Prof. Museru.
 
Aliongeza  kuwa,  hospitali  hiyo  imekua      ikiendelea      kuboresha      huduma  zake  na  kufanikiwa  kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazifanyiki nchini.
 
“Tumeanzisha huduma ambazo zamani  ilikua  ni  lazima  mgonjwa  aende   kutibiwa   nje   ya   nchi,   na   vilevile   tunatoa   huduma   ya   tiba   radiolojia      (Interventinal Radiology),   nia   yetu   ni   kuhakikisha   huduma hizi zinaendelea ili Watanzania wengi wazipate,” alisema.

Alieleza   kuwa      sasa   huduma   hizo  wanaitoa  Muhimbili,  ambapo  wanatoa  huduma  ya  kupandikiza  figo ambapo mpaka sasa wagonjwa 28 tayari wamepandikizwa, watoto 21 wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant).

Mbali   ya   huduma   hizo,   Mkurugenzi  huyo  alifafanua  kuwa  kwa    sasa  wanafunga  MRI  mpya  ili  kuipumzisha iliyopo ambayo imefanya kazi kwa muda mrefu.

Kwa     upande     wake     Katibu     wa  TUGHE  Mkoa  wa  Ilala,  Tabu  Mambo   aliupongeza   uongozi   wa   Muhimbili  kwa  utendaji  bora  wa  kazi  na  kueleza  kuwa  chama  hicho  kinatambua     mchango     mkubwa     unaotolewa na hospitali hiyo katika kuhakikisha   wananchi   wanapata   huduma bora.

Mkutano   huo   ulibeba   ajenda   mbalimbali  ikiwemo  kutoa  taarifa  za  utendaji  kazi  wa  chama  pamoja  na   kutoa   taarifa   ya   mapato   na   matumizi kwa mwaka


from MPEKUZI

Comments