Diamond akabidhi rasmi kadi za bima ya Resolution kwa wakazi wa Tandale

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul, Diamond Platinum ameshakamilisha ahadi yake ya kuwapatia kadi ya huduma ya bima ya afya wananchi wa Tandale.

Diamond aliwahi kutoa ahadi hiyo wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa ya kuwa angewapatia kadi hizo wananchi 1000 wa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwao.

Wakazi hao wamepewa msaada huo wa bima ya afya kupitia kampuni ya bima ya Resolution Insurance ambapo Mkurugenzi Mtendaji wake Maryann Mugo alibainisha kuwa huduma hiyo ni kwa ajili ya watu wanne kwenye familia.

Alisema,”sisi tunapenda kuwahudumia wananchi kujipatia huduma nzuri za afya na kwa kile alichokifanya msanii Diamond kuwasaidia wakazi hawa huduma ya bima basi ni fahari kubwa kwetu”.

Kwa upande wake msanii Diamond aliyewakilishwa na dada yake Esma kwenye makabidhiano hayo aliwataka wananchi wa Tandale kutumia vema huduma za bima hiyo na kujiwekea akiba ya fedha ili mwisho wa siku huduma hiyo ya mwaka mmoja ikiisha waweze kujihudumia kama kawaida.


from MPEKUZI

Comments