UPDATES: RPC Lazaro Mambosasa Asema waliomteka mfanya biashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji

Mambosasa amesema kwamba wameweka vizuizi  kila sehemu kuhakikisha hakuna mtu anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi, na kwamba waliohusika kwenye tukio la kumteka  ni raia wawili wa kigeni.  

Mohammed Dewji, anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto leo saa 11 Alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi Gym ya Colosseum, Oysterbay Dar es salaam.


from MPEKUZI

Comments