Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 03

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
Bibi Jane akanionyesha chumba changu cha kulala, nikaweka begi langu kisha tukarudi sebleni na kupata chakula kilicho andaliwa vizuri sana. Ila muda wote nikajikuta nikimtazama Mery na kujiuliza ni kwa nini amenidharau.
“Mery unatakiwa kumuomba msamaha Ethan kwa kuto kuupokea mkono wake.”
Mzee Klopp alizungumza huku akinimtazama Mery.
“Baba na mama pasipo kuwavunjia heshima siwezi kumuomba huyo sokwe msahama, na inakuwaje munaleta Masokwe nyumbani kwetu na wala hamjanishirikisha eheee?”
Kauli hii, ikaulipua moyo wangu, hasira ikapanda na kunifanya mwili mzima kunitetemeka, glasi ya juisi niliyo ishika mkoni mwangu, nikajikuta ikiniponyoka na kuanguka chini jambo lililo wafanya watu wote kunishangaa.
   
ENDELEA
Nikanyanyuka kwa hasira kwenye kiti changu na kukimbilia chumbani kwangu huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Nikajitupa kitandani na kuendelea kulia, hazikupita hata dakika mbili bi Jane Klopp akaingia chumbani humu, taratibu akaka kitandani na kunikumbatia na kuanza kunibembeleza huku akioniomba niweze kuwa mvumilivu na mtoto wao atanielewa tu.
“Kwa hiyo mimi ni Sokwe?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole na masikitiko mengi sana, japo ni mtoto ila swala la kudharauliwa na kuitwa sokwe kusema kweli limeniumiza sana moyo wangu.
“Hapana Ethan, watu wote sisi ni sawa mwanangu, wala usijisikie vibaya”
 
Bibi Jane Klopp akatumia muda mwingi sana katika kunibembeleza hadi nikapitia wa usingizi. Ubaridi mkali ulioa ambatana na upepo ukanifanya niweze kuzinduka usingizini, nikatazama chumba kizima na kukuta mwanga hafifu wa mbala mwezi unao ingia kupitia dirisha ambalo lipo wazi. Taratibu nikashuka kitandani na kuanza kutembea kuelekea lilipo dirisha hilo ili niweze kulifungua. Kabla sijalifikia sauti ya mwanaume ambaye aliniita kipindi nilipo kuwa hotelini, ikaniita tena nyuma yangu. Nikastuka sana na kugeuka, nikaona kivuli kikiwa ukutani.
 
“Ethan pole sana kwa kile kilicho kukuta”
Sauti ya mwanaume huyu ilizungumza na kunifanya niingiwe na hofu.
“Usiogope, natambua kwamba umefedheheka sana moyoni mwako, ila nina kitu ninahitaji kukuonyesha”
“Kitu gani?”
“Twende nje”
“Nje, wapi?”
Niliuliza kwa kujikaza tu, ila kusema kweli nina wasiwasi mwingi.
“Wewe twende tu”
Nikahisi hali ya kujiamini moyoni mwangu, taratibu nikaanza kutembea kuelekea mlangoni.
“Hapana usipitie mlangoni”
Sauti ya mwanaume huyu iliendelea kunielekeza, na hali ya kuiogopa yote imenitoweka.
“Wapi nipitie?”
“Dirishani pale”
Nikatembea hadi dirishani na kuchungulia nje.
“Nitatokaje hapa wakati kuna gorofa?”
“Wewe ruka hadi chini?”
“Acha kunitania, nitarukaje hadi chini. Unataka nivunjike”
“Kumbuka kwamba nilisha kueleza nipo kwa ajili ya kukusaidia, kwa hiyo siwezi kukuacha uumie”
 
Nikajishauri kwa sekunde kadhaa, akili za utoto nahisi nazo zinachangia, kwani sikuhitahi kufikiria jambo hili kwa mapana na kujaribu kile ambacho nina ambiwa. Taratibu nikapanda dirishani na kujirusha kwenda chini huku nikiwa nimeyafumba macho yangu. 
Kitu kilicho nishangaza ni kuto kufika chini ya ardhi, nikafumbua macho yangu kwa haraka sana. Nikajikuta nikiwa nina ambaa hewani huku chini ya ardhi kukiwa na ukungu mwingi sana kama tulio zoea kuuona Moshi majira ya asubuhi au usiku.
“Usiogope”
“Umefanya nini sasa mbona sikanyagi chini?”
Niliuliza huku mapigo ya moyo yakinienda mbio.
“Unaniamini?”
 
“Ehee…..!!?”
“Unaniamini kama rafiki yako?”
“Nitakuaminije ikiwa sikuoni sura yako”
“Unataka kuniona sura yangu?”
“Ndio”
“Twende”
Tartaibu nikaanza kuona nikiondoka katika eneo nililopo, nikatamani kujifinya ili mardi niweze kuona kama nipo ndotoni au laa, ila kila kinacho tokea ni jambo la ukweli na si ndoto kabisa. Tukazidi kupita juu yam situ huu uliopo karibu kabisa na msitu wa jumba la mzee Klopp na mkewe.
“Tunaelekea wapi?”
“Ninataka kukuonyesha Ujerumani jinsi ilivyo”
“Sasa utanionyeshaje ujerumani ilivyo ikiwa hutaki nikuone sura yako”
“Utaniona tu siku, muda bodo haujafika”
Nikaanza kuona majengo mengi makubwa kwa juu. Majengo haya yote yamejengwa kwa ustadi wa hali ya juu, akaanza kunielezea kila mji na sifa zake pamoja na asili ya watu wake. Kusema kweli ni jambo ambalo linanifurahisha moyoni mwangu na kuniburudisha.
“Kwa nini umekuwa rafiki yangu na unaitwa nani?”
“Hahaaa…..”
Sauti hii ya kiume ilicheka kidogo.
“Jina langu ni gumu sana, nitakutajia siku nyingine”
“Kwa nini?”
 
“Usijali nitakuambia, kuna mambo mengi sana nahitaji tufanye pamoja na yakikamilika basi nitakueleza na utanijua”
“Haya kwa nini umenipenda mimi?”
“Hahaa….niyauambia pia hiyo siku ikifika”
Tukaendelea kuzunguka hadi ilipo kuwa ikaribia majira ya asubuhi, akaniridisha hadi chumbani kwangu, kisha akaniaga na kuondoka jambo ambalo kusema kweli linazidi kunishangaza. Nikapanda kitandani taratibu huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana ya kuiona miji ya nchi hii ya Ujerumani. Usingizi taratibu ukaanza kunipitia na nikalala fofofo.
    Bibi Jane Klopp akaniamsha, akanieleza juu ya safari ya matembezi na kwenda kuiona shule ambayo ninatakiwa kuanza masomo yangu ya shule ya msingi. 
 
“Jiandae”
“Sawa mama”
Nikaingia bafuni, nikajisafisha kinywa changu na kuoga, baada ya kumaliza, nikavaa moja ya suti ya kijivu ambayo bi Jane Klopp alininunulia. Nikatoka chumbani humu na kuelekea sebleni, nikakutana na Mery akiwa amevalia suti nyeusi, nikajaribu kumsalimia ila hakiniitikia zaidi ya kunipita.
“Dada Mery nimekusalimia”
“Wewe nguruwe mdogo nimekuomba salamu yako”
Mery alizungumza huku akinitazama usoni mwangu kwa hasira.
“Nikiwa kama mdogo wako ni lazima nikupatie heshima”
Nikastukia kofi usoni mwangu jambo lililo nifanya nijisikie vibaya sana.
“Mery ni nini unacho fanya?”
Mzee Klopp alizungumza kwa ukali huku akishuka kwenye ngazi.
 
“Nimewaambia huyu Sokwe, sijui nguruwe, sitaki kumuona huku”
“Hiyo sio tabia tuliyo kufundisha sisi wazazi wako lakini?”
Mzee Klopp alilalama kidogo.
“Kwa nini munanikosesha amani eheee, khaa”
Mery akatoka humu ndania kiwa na jazba, mzee Klopp akanifwata nilipo simama na kunikumbatia.
“Ethan, kila kitu kinakwenda kukaa vizuri sawa mwanangu”
“Sawa baba”
Nilijibu huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Nikaanza kuhisi magari yakigongana huku moja likipinduka vibaya sana. Katika ufahamu wangu wa akili nikamuona Mery akiwa ndani ya gari hilo lililo pinduka. Nikatamani kuzungumza hisia zangu ninazo zihisi ila nikashindwa kutokana na kuogopa, nikamuachia mzee Klopp na kuanza kukimbilia nje, kwa mbali nikaliona gari ambalo amepanda Mery likitoka kwenye geti na gari hilo ndio nililo liona kwenye hisia zangu na hii ndio mara yangu ya kwanza kuliona.
 
“Achana naye akirudi jioni tutazungumza naye”
“Baba”
“Naam”
“Nitakacho kuambia utaweza kukiamini?”
“Yaa kwa nini nisikuamini”
“Naomba umzuie dada Mery asiende anapo kwenda?”
“Kwa nini?”
“Ninahisi kuna ajali itatokea?”
“Ajali?”
“Ndio baba”
Mzee Klopp akaonekana kuelewa kile nilicho kizungumza. Akatoa simu yake mfukoni na kuanza kuminya minya, akaiweka sikioni kwa sekunde kadhaa ila akaishusha, akarudia tena kuiweka simu yake sikioni ila baada ya muda mchache tena akaishusha.
“Anakata simu”
Mzee Klopp alizungumza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana. Bibi Jane Klopp akatoka ndani huku akiwa amependeza sana.
“Mbona muna wasiwasi kuna nini kinacho endelea?”
“Ethan muambie mama yako”
Mzee Klopp alizungumza huku akiendelea kumimnya minya simu yake na kuiweka sikioni.
 
“Eti Ethan ni nini kinacho endelea?”
“Ninahisi kuna ajali mbaya itampata dada Mery”
Bibi Jane Klopp wasiwasi mwingi ukamjaa.
“Mume wangu tutafanya nini?”
“Najaribu kumpigia anakata simu, amempiga mtoto wa watu hapa anahisi labda ndio hilo jambo ninataka kuzungumza naye”
“Mpigie dereva wake”
Mzee Klopp akafwata ushauri wa mke wake.
“Ehee upo wapi?”
“Nyumbani…..unafanyaje?”
“Ohooo Mungu wangu haya”
Mzee Klopp akakata simu huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi.
“Alimuambia dereva wake asije leo kazini”
“Mungu wangu, ngoja nijaribu kumpigia mimi”
Bi Jane Klopp akatoa simu yake kwenye pochi, akapiga namba ya Mery, sura yake jinsi ilivyo anza kubadilika dhairi ikaonyesha kwamba kuna tatizo limejitokeza.
 
“Kuna nini mke wangu”
“Nimesikia kishindo kizito na siu ikakata”
“Ohooo…Mungu baba ni nini tena kimempata”
Bibi Jane Klopp akaanguka chini, jambo lililo tufanya tuchanganyikiwe. Wafanyakazi kwa haraka wakafika katika eneo hili na kusaidiana na mzee Klopp kumuingiza ndani bi Jane Klopp. Simu ya mzee Klopp ikaanza kuita, akaitazama kwa muda huku akinitazama usoni mwangu. Akaipokea simu yake na kuiweka sikioni.
“Ndio ni mimi”
Nikamuona Mzee Klopp machozi yakimlenga lenga. Taratibu akaka kwenye kochi akionekana dhairi kwamba amechoka kwa taarifa alizo pewa.
“Sawa ninakuja”
Mzee Klopp alizungumza kwa uonge huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu akanyanyuka na kunishika mkono na tukaanza kupandisha kuelekea gorofani.
 
“Ethan umejuaje kama mwanangu atapata ajali?”
“Eheee?”
“Ulijuaje?”
Mzee Klopp alizungumza kwa ukali kidogo.
“M…imi…nimehisi tu”
“Unahisi umekuwa malaika wewe?”
Mzee Ethan alizidi kufoka hadi sura ikaanza kuwa nyekundu jambo lililo nifanya nianze kupata woga.
“Na akifa mwanangu utanitambua”
“Likini bab…..”
“Koma mimi sio baba yako, mwanangu ni mmoja na anakimbizwa hospitalini sasa hivi unaniambia nini nikuelewe mjinga weweee”
Maneno ya mzee Klopp yakanikatisha tamaa kwa kweli ya kuendelea kuishi humu  kwenye nyumba yake, kwa kweli kwa hapo awali nilihisi kwamba nitayafurahia maisha yangu ya hapa nchini Ujerumani, ila kile nilicho kifikiria sicho kinacho nitokea na nimekuwa ni tatizo toka niingie jana kwenye hili jumba.from MPEKUZI

Comments