Mfumuko wa Bei Mwezi Septemba Wapanda

Mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia Septemba umeongezeka kutoka asilimia 3.3 uliokuwapo mwaka ulioishia Agosti mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inasema kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa Septemba imeongezeka kidogo ikilinganishwa na ilivyokuwa Agosti.

Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo amesema kupanda kwa mfumuko huo wa bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa mwaka huu ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2017.

"Lakini mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba 2018 umeendelea kupungua hadi asilimia 2.0 kutoka asilimia 2.0 ya Agosti," amesema Kwesigabo.

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko la mfumuko ni vileo na bidhaa za tumbaku kwa asilimia 1.9, nguo na viatu (3.2), vifaa vya matengenezo na ukarabati wa nyumba (5.2) na mafuta ya taa asilimia 18.7

Nyingine ni mkaa (11.2), gharama za kumuona daktari katika hospitali binafsi (5.5), dizeli 19.9 na petroli kwa asilimia 15.8.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo amesema mfumuko kwa baadhi ya nchi katika kipindi hicho ni juu ya uliopo Tanzania.

Kwa Kenya umeongezeka kutoka asilimia 4.04 hadi asilimia 5.70 wakati Uganda ukipungua asilimia kutoka 3.8 hadi 3.7 katika kipindi hicho.



from MPEKUZI

Comments