Mahakama yapokea hati ya kifo mshtakiwa kesi ya uhujumu uchumi

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepokea hati ya kifo ya mshtakiwa wa tatu Benjamin Mwakatumbula aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kusababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 1.16, pamoja na wenzake akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) wa zamani, Dickson Maimu.

Mwakatumbula wakati wa uhai wake alikuwa Kaimu Mhasibu Mkuu wa Nida, hati ya kifo chake iliwasilishwa na upande wa utetezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa jana.

Wakili Serikali Imani Mitumizizi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ilipangwa kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, mshtakiwa Maimu aliwakabidhi Wakili wa utetezi Faisal Ali bahasha ya kaki na ilipofunguliwa ilikuwa na hati ya kifo na kuikabidhi mahakama.

Hakimu Mashauri alisema mahakama imepokea hati ya kifo cha Mwakatumbula na mwenendo wa kesi dhidi yake umefutwa.Alisema kesi hiyo itatajwa tena Novemba 15,mwaka huu dhamana ya washtakiwa inaendelea.

Mbali ya Maimu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Biashara wa NIDA, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. 1,169,352,931.



from MPEKUZI

Comments