Kortini Kwa Kukutwa na Miguu Ya Nyumbu

Marwa Itembe (28),  mkazi wa kijiji cha Mbalimbali wilayani Serengeti Mkoa wa Mara amefikishwa mahakamani kwa makosa matatu ya uhujumu uchumi.

Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa Polisi,  Paskael Nkenyenge jana Jumanne Oktoba 9, 2918 alisema  mshtakiwa alikamatwa na miguu miwili ya nyumbu yenye thamani ya Sh1.4milioni.

Akisoma hati ya mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi namba 111/2018 alisema kosa la kwanza ni kuingia ndani ya hifadhi ya Taifa, la pili ni  kupatikana na  silaha za jadi panga na kutega wanyamapori  ndani ya hifadhi kinyume cha sheria.

Alisema kosa la tatu ni kumiliki nyara za Serikali baada ya kukutwa na  miguu miwili ya mnyamapori huyo ikiwa na thamani ya Sh1.4milioni kinyume cha sheria.

Ametenda makosa hayo Oktoba 7, 2018 katika eneo la Nyamburi ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote na  amerudishwa mahabusu hadi Oktoba 23, 2018 kesi hiyo itakapotajwa tena.


from MPEKUZI

Comments