Kahawa yamponza mkuu wa polisi mkoani Kagera....IGP Sirro Amhamisha Kituo Kupisha Uchunguzi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amemhamisha kituo cha kazi kamanda wa Polisi Wilaya ya Kerwa mkoani Kagera, Justine Joseph, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilitolewa dhidi yake na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa madai ya kusafirisha kahawa nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Barnabas Mwakalukwa amesema IGP Sirro pia amemwagiza RPC wa Kagera Augustine Ollomi, kuwachukulia hatua askari wote wa Kerwa, waliohusika na usafirisahaji wa Kahawa kwenda nje ya nchi.

"Kamanda wa polisi wilaya ya Kerwa amehamishwa kituo cha kazi kutoka Kerwa na kupelekwa Iringa ambako atakuwa mtumishi wa kawaida ili kupisha uchunguzi, na atakuwa chini ya usimamizi wa viongozi wengine." Amesema Mwakalukwa.

Aidha IGP Sirro amewataka askari wote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia, sheria na maadili ya jeshi la polisi nchini. 

Mbali na hilo Sirro pia amewataka wananchi kuachana na imani ya kishirikina kwa kuwa vitendo hivyo vinasababisha kuongezeka kwa matukio ya kiuhalifu katika baadhi ya maeneo nchini.

Kauli hiyo ya IGP Sirro imekuja kufuatia vurugu za mkoani Songwe baada ya wananchi kuwazuia askari polisi kuwakamata waganga wakienyeji mkoani humo, maarufu kama 'rambaramba' ambao wamekuwa wakiendesha kampeni ya kufanya ramli inayolenga kuvuruga amani.


from MPEKUZI

Comments