Dr Mengi Kuanzisha Kiwanda Cha Kutengeneza Simu za SmartPhone Hapa Nchini....Simu Zitakuwa na Uwezo wa Kukaa cha Chaji Wiki 2

Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Dk. Regnald Mengi ametambulisha ujio wa kampuni yake mpya ambayo itakuwa ni ya kwanza Tanzania kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali za Kielektroniki, ikiwa ni pamoja na simu za mikononi, simu janja (Smartphones), computers, Ipads, music bluetooth speakers, headphones, earphones .

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dk Mengi amesema simu ambazo zitatengenezwa zitakuwa zinakaa na charge kwa zaidi ya wiki moja zikiwa ni maalumu kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hasa vijijini pia aina hizo za simu zitatumika kama power Bank kucharge simu zingine.

Aidha ameeleza kuwa wanatarajia kutoa ajira zaidi ya 2000 rasmi na zisizo rasmi na kampuni itatoa kipaumbele katika kuajiri wenye ulemavu, wenye sifa stahiki



from MPEKUZI

Comments