Ali Kiba Aguswa na Hali Ya Chid Benz, Ataka Watanzania Tumuombee Aache Madawa ya Kulevya

Msanii wa Bongo, Alikiba amesema kuwa licha ya Chid Benz kutumbukia kwenye matumizi ya Dawa za Kulevya bado anahitajika kwenye muziki huo.

Kwenye Mahojiano na kipindi cha Leo tena cha Clouds FM, Alikiba anaamini Mungu atamfanyia wepesi Chid Benz kuondoka kwenye kifungo hicho na pia anamuombea kwa sasa.

"Namuombea kaka yangu Chid Benz apate uwezo wa kushinda matamanio ya moyo wake, Allah amsaidie aushinde mtihani anaoupitia. Bado tunamhitaji, ana familia inayomtegemea.

"Tumuombee maana kama hatoamua mwenyewe basi hatoweza kutoka kwenye hili shimo. In Shaa Allah mwenyezi Mungu atamfanyia wepes” amesema Alikiba.

Kwa sasa Alikiba anafanya vizuri na wimbo mpya uitwao Mwambie Sina ambao ni kwanza kutoka chini ya lebo yake inayokwenda kwa jina la King's Music.


from MPEKUZI

Comments