Tisa Wakamatwa Pwani Kwa Makosa Ya Kiuhalifu

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la Polisi mkoani  Pwani  linawashikilia watu Tisa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji, wizi na vitendo vingine vya kihalifu.
 
Ikumbukwe kwamba,  septemba 18 majira ya saa 21:15 usiku katika kitongoji cha Kibosho ,Mapinga Wilaya ya Bagamoyo, watuhumiwa 15 wakiwa na gobore, mapanga, nondo na visu walivamia makazi ya  Jaji mstaafu Salum Masati (69) na Flora Timoth (59) muuguzi hospitali ya Mwananyamala-Dar es salaam. 
 
Aidha baadhi ya nyumba za wananchi wa eneo hilo, waliwajeruhi na kuiba pesa taslim, simu wa mkononi aina mbalimbali, laptop, televisheni, ipad, saa za mkononi, spika za music system na vitu vingine vyenye thamani mbalimbali na kutokomea navyo. 
 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa, alisema kufuatia matukio hayo jeshi hilo kwa kushirikiana na raia wema lilipokea taarifa za watuhumiwa wanaojihusisha na matukio hayo.
 
“Septemba  28 kati ya saa 6-8 usiku na tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa (majina yamehifadhiwa) “
 
“Baada ya kufanyiwa upekuzi tuliwakamata na gobore, televisheni 4,deki za video 5, amplifaya 3, ving’amuzi 4, redio za subwoofer 3, spika 5,simu za mkononi za aina mbalimbali 15, bangi ambayo haijasokotwa kifurushi kimoja ,misokoto/kete 169 na pakiti moja ya karatasi za kusokotea iitwayo lizla”alieleza Wankyo. 
 
Aliwataka ,wananchi  wa Mapinga na maeneo ya jirani waliowahi kuvamiwa, kujeruhiwa na kuporwa kufika katika kituo cha polisi cha Mapinga wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutambua mali zilizokamatwa .
 
Wankyo alitoa rai kwa wananchi  kuliamini Jeshi la Polisi na kuendelea kuwapatia taarifa za uhalifu na wahalifu pasipo kusita waweze kukamatwa na sheria ichukue mkondo wake.


from MPEKUZI

Comments