Mashirika Yatakiwa Kuhudumia Jamii Kwa Kurudisha Faida Wanayopata

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Taasisi na mashirika mbali mbali hapa nchini yametakiwa kurudisha sehemu ya faida wanayo ipata ili kuhudumia Huduma za kijamii zikiwemo Mausala ya afya elimu na watoto wasiojiweza Sanjari na maafa mbali mbali

Akizungumza  wakati akitoa msaada kwenye shule ya Msingi na ufundi Sing’isi wilayani Arumeru mkoani Arusha mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani amesema kwamba katika faida wanayo ipata watakikisha wanaendelea kusaidia sekta ya elimu nchini

Aidha ameyataka mashirika mbali mbali kuona namna ya kurudisha faida wanayopta katika kuhudumia masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo kusaidiana na serikali katika hatua mbali mbali za kuwaleta maendeleo wananchi hususani benki hiyo ilipokuwa ikikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 4 katika shule ya msingi na ufundi ya Sing’isi 

Amezitaka taasisi mbali mbali kujitokeza katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya ,kutoa elimu bure na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya awali bila kuwepo na changamoto ya madarasa pamoja na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya kusoma na kufundishia

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Singisi Safira  Ndelwa ametaja changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya majengo katika shule hiyo  ikiwemo uhaba wa vyumba vya kusomea na uzio wa shule

‘’Shule hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uzio uhaba wa vyumba vya madarasa mashine ya kuchapisha mitihani pamoja na nyumba za walimu ‘’alisema mwalimu Ndelwa

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Anjela Izack ameshukuru benki hiyo kwa msaada huo na kuomba kuongezewa madarasa mawili kwa lengo la kuondoa usumbufu wa wanafunzi wenzake kusoma kwa awamu mbili kwani wanachoka na masomo yao na kujikuta wakishindwa kushika masomo na maendeleo kushuka.

Pichani ni Mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani akiwa na mwalim mkuu wa shule ya ufundi na msingi Sing'isi Safira Ndelwa  wakati wa makabidhiano ya Hundi kutoka Benki ya CBA picha zote na mahamoud ahamd Meru

Sehemu ya Wanafunzi wa shule ya msingi na ufundi Sing'isi wakiwa na mfano wa hundi waliokabidhiwa na benki ya CBA jana wilayani Arumeru 


from MPEKUZI

Comments