Ommy Dimpoz Kafunguka Kila Kitu Kuhusu Ugonjwa Wake....Anasema Alilishwa Sumu Bila Kujua

Vipimo  vya afya alivyofanyiwa msanii wa Bongofleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu, vimeonyesha aliwekewa sumu kwenye chakula.

Ommy Dimpoz alianza kuugua mapema Mei mwaka huu na kwenda kutibiwa mjini Mombasa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini ambako aligundulika kuwa na tatizo katika njia ya chakula ambako alifanyiwa upasuaji.

Akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds, Dimpoz, alisema vipimo vya madaktari vimeonyesha tatizo lake linatokana na kuwekewa sumu kwenye chakula ama kinywaji.

“Awali nilifanyiwa vipimo katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam na kugundulika nina kansa, lakini baada ya vipimo vikubwa huku Afrika Kusini, imeonekana nimekula sumu,”  alisema Ommy Dimpoz.

Alisema anashukuru kuona hali yake imeanza kuimarika baada ya awali kushindwa kuzungumza kabisa na anaamini sala za Watanzania wenzake na watu ambao wamekuwa karibu naye zitamsaidia na kuweza kurejea kwenye hali yake.

Akizungumzia kuhusu namna upasuaji wake ulivyofanyika na kusababisha kukaa Chumba cha Uangalizi Maalumu ICU kwa muda wa wiki tatu baada ya mapafu yake kuleta shida, Dimpoz amesema;

“Baada ya kufanyiwa upasuaji kulikuwa kuna matatizo, mapafu yakawa hayafanyi kazi vizuri, kwahiyo baada ya kutoka kwenye upasuaji nikapelekwa ICU (chumba cha wangojwa mahututi) hali ilibadilika kwa sababu upasuaji walisema ni masaa 4 lakini yakaenda mpaka masaa 11. Kwa hiyo nikaa ICU kwa wiki tatu baada ya pale nikahamishiwa wodi ya wangonjwa ya kawaida muda ukafika wakaniruhusu bwana unaweza kwenda lakini unatakiwa kurudi baada miezi 3,”

Kuhusu sauti kubadilika alisema, “Side effect ya upasuaji huu sauti inaweza kwenda na kurudi, kwahiyo hivyo vitu tayari nilishaambiwa. Sometime nakuwa nipo fresh some time ndio inakuwa hivyo lakini wakati nipo mapumzikoni Kenya nilijaribu kuingia studio. Mabadiliko mengine tumbo langu sasa hivi limeamishwa limevutwa juu, kwahiyo hata nikila nashiba haraka nikila kidogo,”

Muimbaji huyo amesema bado hajajua ni sumu ya aina gani ambayo ametumia au amelishwa.

Katika hatua nyingine amesema baada ya kufika hospitali nchini Afrika Kusini safari hii aliwaeleza madaktari jinsi anavyojisikia na kufanyiwa vipimo.

“Walivyonipima wakakuta ndani kuna usaha mwingi sana, akaseama inabidi tukutoboe pembeni ya tumbo tuunyonye, kwahiyo kuutoa siku ya kwanza wakatoa lita moja, wakaendelea mpaka mambo yakakaa sawa,” alisema Ommy.


from MPEKUZI

Comments