Muigizaji wa Bongo Movie, Odama azushiwa kifo

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Jennifer Kyaka maarufu kama ODAMA amezushiwa kifo na watu kwenye mtandao wa facebook.

Odama akielezea kilichotokea ame-screenshot picha za matangazo na kuyaposti kwenye kurasa zake za mitandao ya kujamii na kuujulisha umma kuwa habari hizo sio za kweli.

Odama kwenye maelezo yake amemshukuru mtu huyo aliyemzushia kifo ambapo amedai kuwa kifo kinapangwa na Mungu na muda wake ukifika basi atakufa ila sio kwa kuzushiwa na binadamu.

"KIFO KIPO NA HAKUNA ATAKAEKIKWEPA… KILA BINADAMU ATAONJA MAUTI NA KUKAMILIKA KWA MAISHA YETU HAPA DUNIANI…. LAKINI PIA HATA KAMA HUMPENDI MTU UNAMCHUKIA IWE ALIKUTENDEA UBAYA AU UMEAMUA TU KUMCHUKIA SIO VIZURI KUMUOMBEA KIFO TENA UKAONA HAITOSHI BASI UNAWEKA MATANGAZO MITANDANDAONI…. NAKUSHUKURU WEWE ULIEAMUA KUFANYA HILI.. NAJUA UNANIONGEZEA UMRI WA KUISHI.. NA NIKUAMBIE TU KUA MIMI NI MZIMA WA AFYA NA NINAISHI KWA KUDRA ZA MUNGU.. NITAKUFA TU PALE SIKU YANGU ITAKAPOFIKA MUNGU ATAKAPOAMUA KUNICHUKUA LAKINI SIO KWA KUTAKA WEWE…. SIJUI NILICHOKUKOSEA MPAKA KUFIKIA KUNITANGAZIA KIFO… NAKUOMBEA MAISHA MAREFU ILI UENDELEE KUNIONA NIKIVUTA PUMZI YA MUNGU…. BINADAMU SISI LAITI TUNGELIJUA KUA SI KITU KABISA TUNGEACHA CHUKI ZISIZO NA SABABU…. ASANTE MUNGU KWA KILA KITU."



from MPEKUZI

Comments