Mtoto Wa Jinsia Mbili Ya Kike Na Kiume Azaliwa Muleba Mkoani Kagera

Na Dotto Mwaibale, Kagera
Mtoto wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Geore Kasibante (pichani),  ambaye alisema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospitali  hiyo hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.


from MPEKUZI

Comments