Kamanda wa Polisi Mwanza afunguka kisa cha mtawa kujirusha ghorofa ya tano

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amezungumza na kutaja chanzo cha kifo cha marehemu, Mtawa Bartholomew aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), kilichotokea jana asubuhii mara baada ya mtawa huyo kujirusha kutoka ghorofani ya tano.

Mtawa huyo aliamua kujiuua kutokana na kesi inayomkabili ya upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 380 zilizobainika kupotea.

“Hadi sasa tunaweza kusema kifo chake kimetokana na tukio la upotevu wa fedha katika ofisi yake, akiwa kama mkuu wa kitengo cha fedha tulimkamata na kumhoji kwa siku kadhaa kuhusiana na upotevu huo wa fedha na kumuachia kwa dhamana, hivyo wakati akijirusha kujiua alikuwa nje kwa dhamana,” amefafanua.

Kamanda Shana amesema siku chache kabla ya kifo chake mtawa huyo alikamatwa na kuhojiwa pamoja na watumishi wengine nane ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh milioni 380 za hospitali hiyo.


from MPEKUZI

Comments