TFS Kukusanya Bil. 100 Kuchangia Serikali

Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), imejiwekea malengo zaidi ya kukusanya kiasi cha Sh bilioni 122 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ili waweze kuchangia mfuko mkuu wa fedha za serikali.

Akifunga mafunzo ya siku nne ya kuhusu taratibu za kukusanya maduhuli ya serikali iliyofanyika ukumbi wa VETA mjini hapa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFS Profesa Donsantos Silayo, amesema lengo hilo litatilia mkazo uibuaji vyanzo vipya vya mapato.

“TFS inajivunia na inayo furaha baada ya kuchangia katika mfuko mkuu wa serikali kiasi cha Sh milioni 22.4 baada ya kuvuka lengo lake la kutoa gawio hilo ambalo awali tulipanga kutoa serikali Sh milioni 18.5 kama mchango wao lakini tumetoa zaidi.

“Kwa kweli ni fahari kwetu kama taasisi zilizoweza kuwasilisha fedha hizo katika mfuko huo wa serikali kiasi kwamba tumeshika nafasi ya tano katika utoaji wa gawiwo hilo,” amesema Profesa Silayo.

Akizungumzia mikakati waliyoiweka katika mwaka huu wa fedha, Profesa Silayo amewataka wahasibu kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato vya taasisi hiyo ili kuondoa dhana iliyojengeka kwamba TFS kazi yao ni kuuza mbao na mkaa.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Mhasibu Mkuu wa TFS Peter Mwakosya alisema miongoni mwa changamoto walizonazo ni migongano baina ya wahasibu na maofisa misitu inayosababisha migogoro inayohitaji ufumbuzi wa haraka ili taasisi hiyo iweze kuwndelea kukua katika kipindi cha miaka minane tangu kuanzishwa kuwa wakala wa serikali.

“Migongano hiyo isipotafutiwa ufumbuzi mapema kwa luleta mashirikano baina ya idara zilizomo ndani ya taasisi hiyo, inaweza kuzorotesha ufanisi na kasi iliyojiwekea taasisi katika inapiga hatua na kuwa bora katika kuhudumia wananchi katika shughuli mbalimbali za TFS,” amesema.


from MPEKUZI

Comments