Rais Magufuli Akabidhi Hati Za Viwanja Vya Dodoma Kwa Mabalozi Wa Nchi Mbalimbali Na Wawakilishi Wa Mashirika Ya Kimataifa

Rais John Magufuli amekabidhi hati 67 za viwanja vilivyopo jijini Dodoma kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kujenga makazi na ofisi.

Akikabidhi hati za viwanja hivyo leo Julai 30, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaama amesema Serikali imegharamia kuwalipa watu fidia ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa mabalozi hao.

‘’Leo nyie ni mashuhuda hakuna hata sehemu moja mliyoambiwa muweke saini ,hii ni kwa sababu Serikali yangu imeamua kuwapatia maeneo hayo bure mkajenge ofisi na makazi yenu’’amesema

Amesema  Serikali tayari itahakikisha inatengeneza barabara, ambazo zitafika kwenye maeneo hayo kwa kiwango cha lami, ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma za afya.

Amesema  kwa sasa Serikali karibia yote ilishahamia Dodoma na anayefuata sasa ni yeye ambaye atahamia mwishoni mwa mwaka huu.

“Haikua rahisi kuhamia huko(Dodoma)nawashukuru viongozi wangu kwa ushirikiano wenu mpaka mkakamilisha zoezi hili,’’amesema

‘’Niliona siyo vizuri mimi kuondoka hapa niwaacheni nyie(mabalozi) ndio maana nikaharakakisha mpate hizo hati ili tuhamie wote kwani ilishakuwa historia ya kuhama tangu kipindi cha Nyerere(Mwalimu(Julius) 1973) ni miaka 45 sasa’’amesema

Alisema ametoa agizo wizara husika kutafuta mkandarasi wa kuanza kujenga uwanja wa ndege wa Msalato, wenye ukubwa wa kilomita 3.

“Leo asubuhi nimesema itangazwe tenda ya ujenzi wa uwanja wa Msalato ili ujenzi huo uanze mara moja ili ndege za kimataifa ziweze kutua ikiwamo ndege zetu’’ amesema

Rais Magufuli amewahakikishia usalama mabalozi hao huku akisema Dodoma ni sehemu safi kiusalama na maisha yake pia hayana gharama.

“Mkienda Dodoma mtakaa katika hali ya usalama, kwani hata mkuu wa mkoa kanihakikishia hilo, hivyo ninachoomba tujenge tuhamie kule,’’ amesema

“’Wapo mabalozi wengine walikuwa wakininong’oneza kwamba wataanza ujenzi haraka na mimi nawakaribisha sana mkajenge nyumba mlete pia wawekezaji wa kutosha,’’ ameongeza


from MPEKUZI

Comments