Mapokezi ya ndege mpya ya Boeing 787-800 Dreamliner Jijini Mwanza

Judith Ferdinand, BMG
Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mapokezi (safari ya kwanza) ya ndege mpya  na ya kisasa aina ya Boeing 787-800 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ili kuimarisha shirika la ndege nchini ATCL.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, na kubainisha kwamba ndege hiyo itatua katika uwanja wa ndege wa Mwanza jumapili Julai 29, 2018 majira ya saa moja asubuhi.

Mongella alisema tayari tiketi 244 zimenunuliwa kwa ajili ya safari ya asubuhi na tiketi 158 kwa safari ya usiku hivyo wananchi pia wachangamkie fursa ya kusafiri na ndege hiyo kwa bei nafuu ambapo ina uwezo wa kubeba abiria 262 daraja la kawaida na abiria 22 daraja la biashara.

Kwa upande wake Msimamizi wa kampuni ya ATCL kituo cha Mwanza, Theonestina Ndyetabula  alisema shirika hilo limejipanga vyema na linazidi kuimarika na hivyo kuwahimiza wananchi kutumia ndege zake ikiwemo zile za Bombadier  Dash 8-Q400.

Ndyetabula alisema ndege za Boeing 787-800 Dreamliner pamoja na Bombadier  Dash 8-Q400 zinafanya safari zake mara nne kwa siku katika uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo ndege ya  Dreamliner ya Mwanza – Dar kupitia Kilimanjaro ni saa 09:20 asubuhi hadi 11:40 asubuhi, Mwanza -Dar saa 20:20 hadi  21:40 usiku huku Bombadier Mwanza – Bukoba saa 11:15 asubuhi hadi 11:45 asubuhi na   Mwanza – Dar saa 13:15 mchana hadi 15:00 alasiri.


from MPEKUZI

Comments