Jaji Mkuu Awataka Mahakimu Kutochelewesha Mashauri

Na Magreth Kinabo
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe .Profesa Ibrahim Juma amewataka mahakimu wapya wasiwe chanzo cha ucheleweshaji  wa mashauri.

Aidha   kuacha kulalamika bali pale linapotokea matatizo, bali wawe chachu ya kuyatafutia   ufumbuzi katika utendaji wao wa kazi wa kutoa  huduma  za haki kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Jaji Mkuu huyo wakati akiwaapisha Mahakimu  wapya  kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

“ Kiapo mlichoapa ni uzito muda wote mtakaofanya kazi  ya kuwatumikia  wananchi,  wananchi wanataka kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa haraka,”

Aliongeza kwamba  mfumo wa sasa sio  wa kukaa na kulalamika, kama kuna tatizo litafutiwe ufumbuzi na kuepuka kuwa   chanzo cha ulalamishi.

Alisema  mahakimu hao  wanapaswa kuwa weledi  wanapotoa huduma za utoaji haki ili waweze kutoa hukumu zinazoeleweka kwa kujibu wa sheria na kanuni.  Hivyo wanapaswa kushirikiana na wadau wengine wa mahakama  ili kuahakikisha hukumu zinatoka kwa haraka.

Alisisitiza  mahakimu  hao kwamba kufanya kazi kwa kuepuka rushwa na kwa nidhamu.

Jaji Mkuu huyo  alifafanua kuwa changamoto za majengo chakavu na umbali , visikwamishe  utendaji kazi  wao, hivyo   mahakama iko katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano   ambao unalenga kutoa huduma  za haki kwa wote   na   wakati, ikiwemo  kuboresha miundombinu.

Aliwataka mahakimu hao kuielewa taasisi inayofanyakazi na mpango mkakati huo.  


from MPEKUZI

Comments