CCM Watangaza Kumpokea Rasmi Mwita Waitara....Tazama Hapa Alichokisema Polepole

Chama cha Mapinduzi CCM Kimetangaza kupokea rasmi Maombi ya Mbunge wa jimbo la ukonga kupitia CHADEMA kujiunga na chama hicho muda mfupi baada ya mbunge huyo kutangaza kujivua uanachama na nafasi zake zote kisha kujiunga CCM .

Akizungumza mbele ya vyombo vya habari katika ofisi za makao makuu CCM Limumba jijini Dar- es Salaam , Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole ameeleza kuwa Chama cha mapinduzi kinathamini sana mchango wa mbunge huyu kwani amekuwa ni mbunge anayeamini katika kusimamia ukweli.

Polepole  amesema pamoja na ndugu Mwita Waitara kuacha dhamana ya ubunge, mshahara,  na marupurupu yake, CCM kinatangaza rasmi moja kwa moja kuazia leo hii kitampeleka kwa watanzania kwa ajili ya kusema ukweli wote kwa kuwa ameonesha ujasiri mkubwa kisiasa.

"Wapo wengine ambao wangalikubali wauache ukweli wayaishi maslahi lakini wapo viongozi wachache ambao wapo radhi kupoteza yao ila umma upate kwa hiyo mimi nikupongeze sana ndugu Waitara" amesema Polepole.

Amesema baada ya kupata taarifa za mbunge huyo amezungumza na viongozi wa CCM akiwemo Katibu Mkuu Bashiru Ally, ambaye amempongeza sana Waitara kwa kujiamini kwake na kusimamia ukweli, hivyo CCM itaanza kwenda naye maeneo tofauti kwa hatua ya awali hasa kwenye maeneo ambayo kampeni za uchaguzi mdogo unafanyika ikiwemo jimbo la Buyungu mkoani Kigoma.

Polepole ameongeza kuwa wana-CCM wanayofuraha kushirikiri na Waitara katika kampeni zinazoendelea, na baada ya hapo atapata utambulisho na makaribisho rasmi ya wana-CCM wenzake katika eneo analoishi.

Awali akizungumza mbele ya Waandishi wa habari ndugu Waitara alisema moja kati ya vitu vilivyomuondoa ndani ya chama CHADEMA ni ugomvi wake na Mbowe ndani ya chama.

"Mimi nimeona kabla hawajanipiga chini nijiondoe mwenyewe. Sasa ndani ya CHADEMA, ukionekana na mtu wa CCM unaulizwa kwa nini unaonekana na watu hao. Mimi shida yangu siyo CCM shida yangu ni kuona wananchi wangu wa Ukonga wanatatuliwa shida zao. Wananchi wa Ukonga wavumilie natafuta namna bora ya kuweza kuwa na viongozi wa serikali bila kuhojiwa kama nimefumaniwa na mke wa mtu. Nimetaka kuwa huru" aliongeza. Waitara.

Ikumbukwe kuwa mwaka 1998 Mwita Waitara aliwahi kuwa mwanachama wa CCM  kisha kuhamia CHADEMA lakini leo hii amerejea tena CCM kwa mara nyingine akiwa miongoni mwa wabunge machache machachari wa upinzani waliotikisa kwa hoja nzito katika bunge 11.


from MPEKUZI

Comments