Basata Yasisitizwa Kuwatambua Wasanii Na Kuwaweka Katika Mfumo Rasmi

Na Anitha Jonas – WHUSM
Baraza la Sanaa la Taifa limeagizwa  kufanya kazi kwa bidii  na kuhakikisha linawafikia  wasanii wengi zaidi nchini na ili kuweza kuwatambua na kuwatambulisha kwenye mfumo rasmi.

Agizo hilo limetolewa leo katika kijiji cha Chwamwino Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi alipokuwa akifungua tamasha la kumi la muziki wa Cigogo liliandaliwa na Kituo cha Sanaa Chamwino.

“Tusipotunza Ngoma na Nyimbo zetu siyo tu maarifa yetu yanapotea bali hata utu wetu na historia yetu itapotea kwani jamii nyingi duniani zimepoteza utamaduni wao hivyo ni vyema tulinde na tuenzi utamaduni wetu”Katibu Mkuu Suzan Mlawi.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo Katibu Mkuu huyo alisisitiza suala la wasanii kujiuliza maswali kama wanajitambu na kutambua thamani ya kazi zao na je wanatambua kazi zao za Sanaa ni mtaji mzuri wa kujiletea maendeleo.A

Pamoja na hayo nae Katibu Mtendaji Bw.Godfrey Mngereza alieleza kuwa Tamasha hilo la Chamwino ni chachu katika sekta ya Sanaa kwani linasaidia kujenga kizazi cha sasa na kizazi kijacho kutambua thamani ya utamaduni wao.

“Muziki na Sanaa ndiyo vitu vinavyotumika kututofautisha sisi watu weusi na kupitia tamasha hili linasaidia kutoa elimu kwa watoto namna ya kuthamini muziki wetu na namna Sanaa inaweza kusadia ukuaji wa uchumi”Katibu Mtendaji BASATA Godfrey Mngereza.

Kwa upande wa Mwanadaaji wa Tamasha hilo Dkt.Kedmon Mapana amesema tamasha hilo limeonyesha kukuwa na katika msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka na kufika vikundi Zaidi ya sitini kutoka maeneo mbalimbali nchini na kumekuwa na wageni kutoka nje ya nchi kama Marekani na nchi za jirani.


from MPEKUZI

Comments